SIASA

SAIDI KUBENEA AMSHUSHIA NONDO MAGDALENA SAKAYA

Makamu mwenye kiti kanda ya Dar es salaam ambae pia ni mbunge wa jimbo la Ubungo Mh. Saidi Kubenea amejibu mapigo kutoka kwa Magdalena Sakaya alipokuwa akijibu swali la muandishi wa habari aliyeuliza kuwa ni kweli CHADEMA inataka kukiua chama cha CUF?
Mbunge wa jimbo la Ubungo Said Kubenea akiongea na waandishi wa habari mapema leo kwenye ofisi za kanda Magomeni jijini Dar es salaam na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa kanda ya Dar es salaam Mh. Fredrick Sumaye

Said Kubenea alisema kuwa inabidi ifahamike kuwa Magdalena Sakaya siyo mwanachama wa chama hicho hivyo anashanga kuona akijibu mashambulizi “Magdalena Sakaya alivuliwa uwanachama na kupokonywa cheo cha unaibu katibu Mkuu na baraza halali la CUF na cheo chake kupewa Bw. Bashinge” Alisema Kubenea

Lakini pia CHADEMA ilimsaidia kwa kiasi kikubwa Magdalena Sakaya kupata ubunge kwenye jimbo lake ambalo alikuwa hakubaliki sana na leo hii anamshangaa kuungana na Lipumba ambae harakati zina fanyika yeye alikimbilia Rwanda na kumuacha Maalimu akiwa kiongozi mkuu.

“Na operesheni ondoa msaliti huu ni wakati wake mahususi kwa ajiri ya kumuondoa Lipumba, Sakaya pamoja na genge lao waliloliweka Buguruni kwenye Ofisi kuu za chama hicho. Kwa kuwa waliombwa msaada huo na uongozi wa chama hicho ambacho ni miongoni mwa washirika wenzao wa UKAWA”Alisema Kubenea.
baadhi ya waadishi wa habari wakifuatilia mkutano kwa makini

Hivyo basi kamati kuu ya chama cha CHADEMA vimeamua kwa pamoja kushirikana na Maalim Seif Hamad ambae ni Katibu mkuu wa CUF kumtoa Lipumba na kusema kuwa serikali ya chama cha Mapinduzi ndio inataka kukiua chama cha CUF na wao hawatalifumbia macho swala hili kwani baadae watataka wakiue na CHADEMA ili nchi isiwe na upinzani swala ambalo hawatalikubali.


About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.