Saturday, July 15, 2017

Shule 10 Bora Matokeo Kidato cha 6

Matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15 huku shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys, iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.
 Shule nyingine  ni  Marian  Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.

No comments: