HABARI ZA KIJAMII

TGNP MTANDAO KUANDAA TAMASHA LA 14 LA JINSIA DAR ES SALAAM

TGNP mtandao ipo kwenye maandalizi ya Tamasha la 14 la Jinsia litakalo fanyika tarehe 5 mwezi 8, 2017. Tamasha hilo linalofanyika kila baada ya mwaka mmoja na linawakutanisha wadau mbalimbali toka toka Serikalini, vituo vya taarifa na maarifa, Club za shule tofautitofauti na wanaharakati mbalimbali ngazi ya kata mpaka taifa na wenyeji washiriki wa semina za jinsia(GDSS).
Afisa program wa harakati na nguvu za pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Anna Sangai akitoa ufafafanuzi juu ya jambo fulani kwenye Semina ya maandalizi ya Tamasha la 14  jinsia litakalofanyika Mabibo jijini Dar es salaam
Akiongea kwenye semina jana jumaa tano Bi. Anna Sangai alisema kuwa Tamasha hilo ni la wazi na linawakaribisha watu wa aina zote kwani hakutakuwa na kiingilio hivyo watu wajae kwa wingi kuja kujionea bidhaa mbalimbali za Tanzania na kupata elimu juu ya ukatili wa kijinsia.


Na kauli mbiu ya mwaka huu ya Tamasha hilo inasema “Mageuzi ya mfumo kandamizi kwa usawa wa jinsia na maendeleo endelevu
Bi. Anna Sangai akitoa maelekezo kwenye semina ya wanaharakati wa maendeleo jana kwenye Ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam
Lengo kuu la tamasha hilo ni kusherehekea mafanikio, kujadili changamoto na kubadilishana uzoefu kutokana na harakati wanazozifanya ndani ya muda husika, hivyo wanapokutana inakuwa wakati muafaka wa kupata mrejesho wa kile walichokivuna au wapi wamekwama ndani ya mwaka uliopita.

Miongoni mwa malengo mengine ni kujadili Mikataba ya kimataifa amabyo serikali imeingia  na kuangalia kama utekelezaji wake unafanyika juu ya haki za watoto na wanawake, pamoja na upatikanaji wa huduma muhimu za jamii kama Maji, Elimu, Afya na mengineyo.

Na kwenye Tamasha wageni watakaohudhuria wataweza kupata Elimu bure, Burudani ya ngoma, Ngonjera , Mashairi, Maigizo maonesho ya bidhaa mbalimbali pamoja na makablasha yenye mafunzo mbalimbali ya kupinga ukatili wa kijinsia na utatuzi wake.
Baadhi ya washiriki wa Semina za maendeleo wakifuatilia kwa umakini semina iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam
Lakini pia Bi. Anna Sangai alisisitiza kwa kusema kuwa safari hii wanahitaji bidhaa zinazotengenezwa kwa kazi ya mikono za Watanzania na siyo kuleta bidhaa za viwanda vikubwa au za kutoka nje ya nchi, kwani lengo la tamasha hili ni kutangaza na kukuza soko la bidhaa za ndani kwani watakuwepo wageni toka mataifa mbalimbali ya jirani.

Na kwa wajasiriamali watakaobahatika kuleta bidhaa zao mwaka huu watapata bahati ya kutembelewa na SIDDO kwa ajili ya kupewa utaalamu wa kuboresha bidhaa zao, pamoja na TBS kwa ajili ya kuwapa maelekezo yakufanya namna ya kufungasha ili waweze kuingia kwenye soko la ushindani la bidhaa za ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya wasiriki wa Semina za maendeleo (GDSS)
Na kwa watakao hitaji kupeleka bishaa zao kwenye maonesho hayo ambao ni nje ya wanaharakati wa semina za jinsia(GDSS) wanaombwa kuwasilisha maombi yao mapema kwa kufika makao makuu ya mtandao wa jinsia TGNP yaliyopo mabibo karibu na chuo cha NIT jijini Dar es salaam.About vicent macha

Post a Comment
Powered by Blogger.