Sunday, August 13, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA ZANZIBAR


Benki ya KCB ikifanya ziara katika kituo cha Montessori School and Orphanage.

Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Bi Zuhura Sinare Muro akikabidhi vyakula na vifaa vya malazi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku. Makabidhiano hayo yalifanyika katika kituo hicho, Zanzibar.



Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Bw. Cosmas Kimario (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyakula na vifaa vya malazi vyenye thamani ya shilling 2,963,000 katika kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage, Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro, Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku (wapili Kushoto), Mkuu wa masoko na mahusiano Bi, Christine Manyenye (wakwanza kulia) na Mkuu wa huduma za kibenki za Kiislamu Bw. Rashid Rashid (wakwanza kushoto)

Uongozi na wafanyakazi wa Benki ya KCB kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku (waliokaa, watatu kushoto) na watoto wa kituo hicho.

Baadhi ya watoto wa Montessori School and Orphanage wakitoa burudani kwa uongozi wa benki ya KCB.

Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku (wapili Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuishukuru Benki ya KCB kwa mchango wao katika kituo hicho.

Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyakula na vifaa vya malazi vyenye thamani ya shilling 2,963,000 katika kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage, jana Zanzibar. 

 
 Benki ya KCB Tanzania imekabidhi misaada mbalimbali kwa kituo cha watoto yatima Montessori School Orphans Organization kisiwani Unguja.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Bw, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Bw. Kimario alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

Alisema ni vyema jamii ikatambua uwepo wa watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo, kwa kuwapatia mahitaji mabalimbali kama wanavyopata watoto wa majumbani kwani ni haki yao ya msingi. “Tukiwajali hawa watoto hata kwa Mungu tunapata dhawabu kwani wengi wao hawajapenda kuwa katika mazingira haya” alisema Kimario.

Bw. Kimario, Alielezea kuhusiana na programu endelevu inayoitwa KCB 2jiajiri, na kusema; “KCB 2jiajiri ni programu inayowapa elimu ya nadharia na vitendo wanawake wajasiriamali nchini. Zanzibar, KCB 2jiajiri imefundisha wanawake 32 darasani na maafisa wetu watatu ambao ni wa masoko, fedha na sheria wanazitembelea biashara za wakinamama hao ili kuwapa elimu kwa vitendo.”

Benki ya KCB ilikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo magodoro, mashuka, neti na vyakula.vyenye thamani ya shilling 2,963,000. Mwenyekiti wa bodi ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro alielezea kuhusiana na mchango wa benki hiyo Zanzibar na kusema “Benki ya KCB mbali na kufanya biashara imekuwa ikijihusisha katika miradi mbalimbali yenye manufaa kwa wazanzibari wahitaji.”

Bi. Muro alizitaja baadhi ya michango iliyotolewa na benki hiyo ili kuinua hali ya maisha ya wananchi wenye shida kuwa ni; ujenzi wa kisima cha maji Mazizini Orphanage Centre, utoaji wa vyakula mbalimbali kwa Zanzibar Hayunani Association, vifaa vya kusomea na kuandikia katika shule ya Bwefum na vifaa tiba katika  hospitali za Kivunge Cottage, Mwembeladu na Kombeni. Kwa misaada hii yote Benki imetumia zaidi ya milioni 100.
Mkurugenzi wa kituo cha Montessori School Orphans Organization Susan H. Maziku aliishukuru benki ya KCB kwa mchango wake katika kituo hicho na kuwataka makampuni na jamii kuiga mfano huo wa kuwakumbuka watoto yatima wenye uhitaji mkubwa sana.

No comments: