Thursday, August 10, 2017

TGNP MTANDAO KUZIVALIA NJUGA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WATOTO WA KIKE KWENYE SWALA LA KUPATA ELIMU

Wazazi na walezi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao na kujenga tabia ya kuzungumza nao kuwashirikisha kwenye mambo mbalimbali hususani afya ya uzazi ili kuwalinda na kuwasaidia kupambana na changamoto zinazowakabiri wawapo majumbani na waendapo mashuleni na sehemu nyingine.
Mshauri muelekezi wa mambo ya Jinsia Bi. Agness Lukanga akiongea na washiriki wa Semina za Jinsia(GDSS) mapema jana kwenye semina iliyofanyika makao Makuu ya Mtandao wa Jinsia (TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam
Hayo yamesemwa jana na washiriki wa Semina za GDSS zinazofanyika kila jumaa tano zinazoandaliwa na Mtandao wa Jinsia TGNP, lengo likiwa ni kuwakutanisha wakazi mbalimbali wa kata za jiji la Dar es salaam kujadili changamoto zinazowazunguka ndani ya jamii yao na namna ya kuzitatua.

Na jumaa tano hii mada ilikuwa ni kujadili “Changamoto mbalimbali wanazokutana nazo watoto wa kike kwenye idara ya elimu”.
Baadhi ya washiriki wa Semina GDSS wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji wa Semina hiyo Bi. Agness Lukanga akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema jana jijini Dar es salaam
Kwa mujibu wa washiriki wa semina imeonekana kuwa changamoto kubwa ni Uchumi hii inatokea pale mzazi anaposhindwa kumtimizia mahitaji muhimu mtoto wake, hivyo mtoto inamlazimu kuyatafuta kwa njia nyingine ambayo ni mbaya kama kuwa nawanaume waliomzidi umri hali inayosababisha kupata mimba au kuambukizwa Magonjwa ya zinaa kama Ukimwi.

Lakini pia Malezi mabaya yanachangia kumuharibu mtoto na kwa hali ya sasa ambayo kila mzazi anakuwa yuko bize na mambo yake ya kutafuta pesa bila kujari mtoto kama anaenda shule na pia kufuatilia nyendo na maendeleo ya mtoto wake, hivyo walio wengi hushtuka mtoto akiwa tayari ameshaharibika uenda kapata mimba au kawa na tabia zisizokubalika kwenye jamii.
Bi. Tatu Kitenge akitoa hoja yake kwenye semina  ya GDSS iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia(TGNP) mapema jana jijini Dar es salaam
Utandawazi pia ni changamoto kubwa kwani wanafunzi wa sasa wanamiliki simu kubwa(smart phone) na wazazi wanashindwa hata kuwahoji watoto wao kama hizo simu wanazitoa wapi? Lakini pia wanafunzi hao hao hutumia simu hizo hizo kuangalia picha za ngono na kuangalia vitu vingi vya kutoka nje ambavyo ni tofauti na maadili yetu wa afrika.

Kushindwa kuenzi Mila na Desturi za zamani pia ni tatizo kwa watoto wa sasa kwa kuwa zamani ulikuwa ukikosea mtu yeyote mkubwa anakukanya ikiwezekana kuchapwa, lakini kwa sasa hata ukimkuta mtoto wa jirani yako anafanya mambo yasiyofaa ukijaribu kumkanya kwa kumchapa, mama yake anakuja juu na inawezekana hata ukapelekwa kituo cha polisi na ukamlipa pesa kwa kosa la kumpiga mtoto hali inayowapa watoto wa sasa kiburi.
Bw. Oscar Raphael akitoa maoni yake kwenye Semina iliyofanyika mapema jana kwenye ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Dar es salaam
Lakini pia Sharia zimekuwa zikiwapa kiburi watoto hasa wakike ukimpiga anaweza kukufungulia kesi mahakamani na ukafungwa kutokana na nasheria zinazomlinda mtoto. Lakini huenda ulikuwa na lengo zuri kwa huyo binti la kutaka asipotee kimaadili, au pia ulimkuta sehemu isiyostahili kwa muda huo labda muda wa darasani yeye kaka kijiweni na wahuni, au yupo kwenye kichochoro na baba aliyemzidi umri kwa lengo la kumrubuni  lakini ukimuadhibu sharia inakufunga kwa kosa la kumpiga mtoto.

Vishawishi vya ngono ni miongoni mwa sababu inayokwamisha watoto wa kike kupata elimu hasa kwa wale wanaosoma shule za mbali, wanashawishiwa na makondakta pamoja na madereva wa dala dala pamoja na madereva wa boda boda kwa kuwapa lifti au fedha wanafunzi hao na baadae kuwataka kimapenzi.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Umoja Jesca Saimoni akitoa maoni yake kwenye Semina ya GDSS iliyofanyika mapema jana kwenye ukumbi wa Mtandao wa Jinsia(TGNP) Mabibo jijini Dar es salaam
Lakini pia mashuleni kuna baadhi ya walimu ambao sio waaminifu wanawataka wanafunzi kwa kuwatishia kuwapa adhabu au kuwapa matokeo mabaya kwenye mitihani yao hali inawafanya wanafunzi waoga kukubali na matokeo yake kuwaharibia maisha kwa kuwapa mimba au virusi vya Ukimwi.

Ugomvi mpaka kufikia kutengana kwa wazazi hii inamuweka kwenye nafasi mbaya mtoto wa kike, pale anapokenda na mama yake na baadae baba wa kambo anamtaka binti huyo kimapenzi, au kupelekwa kwa ndugu kama mjomba na baba mdogo na hatimaye binti huyo kunyanyaswa au kufikia kubakwa na hao hao ndugu zake.





No comments: