Friday, August 18, 2017

TIB Corporate bank (TIB CBL) tupo Tanga katika jukwaa la biashara,

 Jukwaa hili limewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na kuona namna gani kila mmoja atawezesha mkoa wa tanga katika kuleta maendeleo.
Theresia Soka Mkuu wa Masoko na Mahusiano TIB Corporate Bank akiwasilisha mada katika jukwaa la biashara mkoa wa Tanga katika ukumbi wa Regal Naivera
TIB Corporate Bank ni benki ya biashara inayotoa huduma zote za kibenki. kwa kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wa Tanga, benki imejiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga. tunatambua kuwa maendelao yoyote yale yakibiahara yanahitaji uwezeshaji wa kifedha (Bank facilities)

TIB Corporate Bank inatoa huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya mteja baadhi ya huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati,dhamana za kibenki (bank guarantee), ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni, uwezeshaji katika hati fungani(treasury bill & bonds) ukusanyaji wa fedha na uwezeshaji wa malipo ya jumla makampuni(cash management) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa njia rahisi na haraka.
Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate bw. Frank Nyabundege akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika jukwaa la biashara lililofanyika mkoani Tanga.
Huduma zetu zote hutolewa kwa umahili na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha mteja anafurahia mahusiano yake na benki . pia huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.


No comments: