NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka Jiji la Shanghai nchini China na kujadili mambo mbalimbali yamaendeleo jijini hapa ikiwemo suala la uboreshaji wa kituo cha Mabasi Ubungo.
Ugeni huo uliambatana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang ambayo ndiyo imeingia mkataba na Halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita alisema kuwa ugeni huo umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali ikiwemo kituo cha mabasi ubungo.
Alifafanua kuwa jiji la Dar es Salaam linakaribia kunza kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kubadilisha kituo cha mabasi ubungo na kwamba hatua mbalimbli zimeshakamilika ili kupisha mradai huo.
Alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo jumla ya watanzania 20,000 watapata ajira jambo ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwezesha vijana kuondokana kwenye makundi ambayo sio salama.
Alisema kufanikisha kwa mradi huo, utasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha jijini hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.
“ Leo nimekutana na ugeni ambapo kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa wamekuwa na urafiki mkubwa katika nchini yetu, tumejadiliana mambo mengi ambayo yote ni yakuleta maendeleo katika jiji letu.
“ Lakini kubwa zaidi ni kuhusu ujenzi wa kituo cha mabasi Ubungo, ambapo hivi karibuni tunatarajia kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia watajulisha, nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa jiji linafuata utaratibu katika kutekeleza mradi huo” alisema Meya Mwita.
“ Fursa hii ni kubwa ambayo tumeipata, watanzania watapata ajira, mzunguko wa fedha kwenye jiji letu utaongezeka, kama Meya wa jiji hili nimewakaribisha tufanye kazi pamoja, lengo likiwa nikuweka jiji kwenye muonekano mzuri” aliongeza.
Kwaupande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya Linghang Cathy Wang alimpongeza Meya Mwita kutokana na aina ya utendaji wake wa kazi nakuahidi kuonyesha ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo.








Makamu wa Rais wa Itel Mobile Bw.Leslie Ding akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.
Balozi wa Itel Mobile,Irene Uwoya akizungumza na wadau pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuanzimisha maadhimisho ya Miaka 10 ya Kampuni hiyo.
Miaka 10 iliyopita Itel Mobile ilizindua mpango wa kumwezesha kila mmoja kuwa na simu bora kwa ajili ya mawasiliano ya uhakika,katika kipindi hicho chote tumepitia katika kipindi kigumu katika Nyanja za kiuchumi na kisiasa lakini tumeweza kufanikiwa kutimiza mlongo mmoja kwa uthabiti mkubwa.
Aidha nguvu kubwa yetu inatokana na bidhaa zetu zilivyo bora pamoja na timu ya wafanyakazi wetu ambao kila mmoja amekuwa akijituma kutokana na nafasi yake na pia ubora na mvuto wa bidhaa unatokana na mapendekezo ya watumiaji wetu na huduma za matengenezo baada ya mauzo na warantii ya miezi 12 kwa bidhaa zetu zote.
Hata hivyo tumekuwa na ushirikiano na mastaa wa nchi za Afrikia kama mabalozi wa kampuni yetu na wamekuwa kiungo muhimu katika kuleta ufahamu na uelewa kuhusu kampuni ya Itel ambapo imekuwa kampuni 3 bora barani Afrika.
Tunaposherekea miaka 10 tunatarajia kuleta mabadiliko makubwa zaidi ili kuimarisha bara la Afrika kwa kutoa bidhaa bora za mawasiliano na leo tunazindua simu mpya ambazo ni za kisas zaidi yaani Itel S12 na S32 na zina ubora kutokana na kuwa kila simu simu ina kamera mbili za mbele pia mwonekano mzuri na kusaidia kuchukua selfie ya kundi ambayo ina uwezo wa kuchukua watu wengi zaidi pia zina Fingerprint ‘alama za vidole’.







