Thursday, September 21, 2017

BAADA YA LHRC KUNYIMWA KUANDAMANA SIKU YA AMANI DUNIANI,WAMEJITOKEZA NA KUZUNGUMZA HAYA MBELE YA WANAHABARI

Kituo cha sheria na haki za Binadamu lhrc kimeviomba vyombo vya ulinzi na usalama nchini  kuwachukulia hatua kali watu wote wanaoshiriki katika vitendo vya uhalifu.

Ombi hilo limetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dkt Hellen Kijo Bisimba wakati akitoa tamko la maadhimsho ya siku ya amani duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi Hellen Kijo bisimba akizungumza na wanahabari kwa niaba ya mashirika 103 ya haki za binadamu nchini katika kuadhimisha siku ya amani Duniani
Dkt hellen amesema endapo vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya watu nchini vitafumbiwa macho vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Aidha Bi Kijo amewataka wananchi kutambua kwamba wao ndio walinzi wa kwanza wa amani nchini hivyo wanapaswa kufuata sheria na kuepuka vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo Mapema leo
Kila ifikapo septemba 21 dunia huadhimisha siku ya amani duniani ambapo kwa mara ya kwanza iliadhimishwa mwaka 1981 baada ya kuidhinishwa na mkutano mkuu wa umoja wa mataifa ikiwa na lengo la kuimarisha wazo la amani ndani ya baraza la umoja wa mataifa.

Katika kuadhimisha siku hiyo Kituo Hicho kilijipanga kufanya maandamano ya amani kuahamasisha amani Nchini lakini kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi hellen Kijo Bisimba,Jeshi la polisi liliwanyima Kibali cha kufanya hivyo kwa kile kilichoitwa kuwa na Viashiria vya uvunjifu wa amani

Kauli mbiu ya siku amani duniani kwa mwaka 2017 ni “pamoja kwa ajili ya amani, nidhamu, usalama na heshima kwa wote”

No comments: