Friday, September 15, 2017

Rasmi wanawake wa Kiislamu kuolewa na wasiokuwa waislamu

Rais wa Tunisia ametangaza kwamba, wanawake sasa wako huru kuolewa na wanaume wasio waislamu.
Image result for wedding ceremony in tunisia
Tangazo hilo limetolewa mwezi mmoja baada ya Rais Beji Caid Essebsi, kutoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo ya mwaka 1973.


Hadi sasa mwanamume ambaye si muislamu anayetaka kumuoa mwanamke wa Tunisia, alihitaji kubadili dini na kuwa muislamu na kutoa cheti cha kuonesha kuwa amefanya hivyo.

Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Tunisia yamekuwa yakifanya kampeni ya kutaka kuondolewa marufuku hiyo wakisema kuwa inakiuka haki za binadamu za kumchagua mke au mume.

No comments: