Wafanya
biashara wa mipakani wametakiwa kuwa wabunifu na wenye hekima na kauli nzuri zitakazo
wavutia wateja wao, na kujaribu kuchunguza soko linahitaji nini kwa wakati
iliopo kabla ya kupeleka bidhaa sokoni.
Hayo
yamesemwa na mwalimu wa biashara na masoko kutoka chuo cha biashara CBE Bi.
Rehema Tambwe alipokuwa akiongoza warsha ya mafunzo kwa wafanya biashara wa
mipakani mapema leo jijini Dar es salaam.
Warsha hiyo
itakayodumu kwa muda wa siku tatu imelenga kuwajenga wafanya biashara wanawake
wa mipakani kwa kuwapa elimu itakayowaongoza kufanya biashara zao kwa uhuru,
uwazi na kwa kujiamini kwa kuwa wanazijua sharia na haki zao za msingi wafikapo
katika mipaka hiyo.
Bi Rehema
alisema kuwa wafanya biashara wengi wamekuwa waoga kuhoji wafikapo mipakani hivyo
kusababisha kupoteza haki zao za msingi, na hii sio kwa wale ambao hawajapata
elimu bali hata kwa wale waliosomea mambo haya ya biashara wakifika eneo hilo
utetemeka na hivyo wasimamizi wa hapo wanawapeleka wanavyotaka wao.
Na hii
inatokana na kutoamini bidhaa yako ama kile ambacho unakwenda kukifanya katika
hiyo nchi unayokwenda kwani ukiwa na bidhaa nzuri imewekwa katika vifungashio
vizuri na pia unajua sharia za umoja wa soko la Afrika Mashariki hautapata tabu
ya kuyumbishwa na yeyote na wala haitakulazimu kuhitaji kutumia njia za panya.
Lakini pia
wafanya biashara wengi wanafanya biashara bila kufanya uchunguzi wa kuangalia
soko linahitaji nini kwa sasa, ama huku ninapopeleka bidhaa wateja wangu ni
wakina nani na matokeo yake wanajikuta wanapeleka bidhaa ambazo zipo kwa wingi
katika eneo hilo na inawezekana zikawa na ubora mkubwa kuliko za kwao na kusababisha
kutonunuliwa kwa bidhaa hazo.
Muwezeshaji aliendelea
kusisitiza swala la ubunifu ni muhimu katika biashara kwani mnapokuwa wafanya biashara
wengi kinachoweza kukutofautisha wewe na wengine ni ubunifu wako katika bidhaa
hata katika muundo wako wa kutoa huduma unahakikisha kuwa unafanya kitu cha
ziada kuhakikisha wateja wanaacha kwenda kwa wengine na wanakuja kwako.
Na jambo
lingine alilolisema muwezeshaji ni kuongeza Thamani katika bidhaa na hii inatokana
na jinsi ya kuziweka bidhaa zako kwa mfano wauzaji wa batiki unapozitengeneza
batiki zako unatafuta vifungashio vizuri unaziwaka hata mteja akija anazidi
kuziona mpya na siyo unaweka kwenye msumari tu zinakuwa na vumbi mpaka mteja
akitokea zinakuwa zimesha chakaa inamlazimu aende akafue ndipo aweze kuivaa.
Bi Rehema
aliendelea kusisitiza kuwa biashara inatakiwa kujiendesha yenyewe na sio
majukumu yako binafsi ukayaingiza katika pesa ya biashara kwani utaanguka tu,
kwa waliowengi wanachukulia fedha zote ni za kwao kwaiyo wanafanya matumizi
bila kujua kuwa wanadidimiza mtaji kwa kuitumia pesa ya biashara katika
matumizi binafsi na matokeo yake umepeleka bidhaa nchi jirani lakini unarudi
msingi ukiwa umepungua.
Na mwisho
kabisa ni swala la mapokezi kwa mteja na kutumia lugha nzuri kwa mteja
itakayomshawishi kununua bidhaa hata kama ajapanga kununua bidhaa hiyo, kwani
ukimpokea vizuri na kwa unyenyekevu na kumpa maneno matamu atavutiwa na biashara
yako na atakuletea wateja wengi zaidi na hii ni kwa kuona ukarimu wako katika
biashara.
No comments:
Post a Comment