Taasisi ya Children Dignity Forum (CDF) wazindua mradi wa “Tuwezeshe”
unaolenga kuwapa uwezo wasichana kuwa viongozi na wajasili katika kutatua
changamoto zinazowakabili katika mustakabali wa maendeleo yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa CDF Bw.Koshuma Mtengeti akizungumza na wanufaika wa mradi huo mara baada ya kumaliza mafunzo hayo |
Akitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es salaam katika
ukumbi wa Double View,Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Koshuma Mtengeti
amesema ili kumpa uwezo wa kuongoza mwanamke basi ni lazima awe jasili na
mwenye kuweza kukabiliana na changamoto na hilo ndio lengo kuu la mradi huo.
“lengo kubwa la project hii ni kumpa uwezo msichana
kuwa kiongozi jasili na mwenye uwezo wa kukabiiana na changamoto”.alisema.
Aidha,Bw.Mtengeti amesema mradi huo ulioanzishwa
mwaka huu utadumu kwa miaka 4 ukiwa na wasichana 16 toka mikoa ya Dar es salaam
na Mwanza utawasaidia wasichana kuwa viongozi majasili na wenye kuweza kutatua
changamoto ambazo mara nyingine zimekuwa zikikatisha ndoto zao.
Mwenyekiti wa bodi ya CDF Bi. Fortunata Temu akitoa neno kwa washiriki 16 ambao watahusika na mradi wa Tuwezeshe. |
Pia, Mwenyekiti wa Bodi ya CDF, Bi.Fortunata Temu
aliwataka wasichana wote waloshiriki katika mafunzo ya mradi huo wakatekeleze yale
walojifunza kwani huo ndio msingi katika kufikia maadhimio ya mradi.
“Nawaombeni sana wote mloshiriki mafunzo haya
yasiishie hapa mkafanye yale mlofundishwa kwani huo ndio msingi mkubwa wa maadhimio
ya mradi huu.”alisema.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mradi huo
akiwemo Bi.Lulu Urio,Mariana Mubelwa na Euphoria Edward wamewashukuru wale wote
walioandaa mafunzo hayo wakiwemo FORWARD UK, AMWA na Mwenyeji CDF kwa kuweza
kuwaletea mradi huo kwani wanaamini ni kama wamezaliwa upya baada ya kupata
mafunzo hayo kwani mbali ya kuongeza marafiki wapya ila kuna kitu kipya
kimeingia ndani ya vichwa vyao na wanaamini havitafutika kamwe mana sasa
wamekuwa majasili na kuweza kusimama na kuongea mbele za watu bila hofu tofauti
na awali.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao wa CDF, Forward Uk na Amwa baada ya kumaliza mafunzo hayo. |
Hata hivyo,Mradi huu wa “Tuwezeshe” umeanzishwa mwaka jana 2016 katika nchi za Uingeleza,Uganda,Kenya,Somalia na mwaka huu ni Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali inayosimamia haki za watoto na kuwawezesha wasichana (Children Dignity Forum).
No comments:
Post a Comment