Sunday, October 8, 2017

JIFUNZE AINA ZA NGIRI NA MATIBABU YAKE

Kuna magonjwa ya hernia ya aina nyingi kama zile ziitwazo kitaalamu inguinal, umbilical, femoral, epigastric, incisional, inguinal hernia na diaphragmatic hernia.
     Image result for DOCTOR PICTUR
Lakini watu wengi hukumbwa na hernia iitwayo inguinal hernia ambayo hutokeza karibu kabisa na sehemu ya siri ambako hapa kimrija kinachochukua mbegu za kiume kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye tumbo na kuingia kwenye kiungo cha kiume.

Hapa panaweza kuwa na uwazi na uwazi huo ukaingia utumbo mdogo na kusababisha hernia hii. Aina hii ya hernia kama nilivyosema hapo juu ndiyo inayosumbua sana watu wengi duniani. Kuna aina nyingine ya hernia inayoweza kutokea kwenye kitovu, sehemu ambayo kunakuwa na mshipa unaopitisha damu yenye chakula na hewasafi ya oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni.

Sehemu hiyo mtoto anapozaliwa panaweza pasijifunge vizuri, hivyo mtoto huyo kupata hernia hii baadaye kwani utumbo mdogo huingia katika kijinafasi hicho kisichojifunga vizuri, hivyo kusababisha uvimbe wa hernia hii. Lakini tatizo hili ikiwa mtoto amezaliwa na akaishi zaidi ya miaka miwili bila kujitokeza tena, basi atakuwa salama kwa sababu kwa muda huo sehemu hiyo huwa imejifunga kabisa.

TIBA
Ikitokea sehemu hiyo ikaacha kujifunga kwa kipindi hicho cha miaka miwili, basi daktari huamua kumfanyia upasuaji mtoto huyo. Kwa watu wazima hernia kwenye kitovu ambayo kitaalamu huitwa umbilical hernia inaweza ikatokea kwa akina mama wenye mimba au kwa wale ambao ni wanene kupita kiasi kwani presha kwenye tumbo inakuwa kubwa na kufunga sehemu hii ya kitovu ambayo inawezekana awali ilikuwa wazi.

Hernia nyingine huweza kutokea kwenye kiungo cha njia ya kumezea chakula kinapoungana na tumbo. Kama sehemu hii haikufunga vizuri utumbo unaingia kwenye kinafasi hicho na kujitokeza kwenye kimfuko kilichopo kifuani kinachoitwa kitaalamu diaphragm.

Ndiyo maana hernia hii huitwa diaphragm hernia.
Hernia nyingine iitwayo femoral hernia hutokea pale mishipa ya damu iendayo kwenye mguu inapopita kwenye tumbo na ikiwa kwenye maungio pana nafasi basi hernia hii hutokea kwenye paja karibu na kiunoni.

Kuna hernia ingine inayotokea kwenye chembe ya moyo ambapo misuli inaachia na kusababisha kingozi cha tumbo na utumbo kuingia katika sehemu hiyo hivyo kuvimba na kusababisha hernia.

Tiba za uhakika za hernia ni kufanyiwa upasuaji kama tulivyofafanua hapo juu.

======

UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata wanaume na wanawake wa rika zote. Mshipa wa ngili ni jina linalokusanya magonjwa kama Ngiri kavu (Hernia), Ngiri maji (Hydrocele) na Ngiri nyinginezo kama vile kuvimba kokwa au mfereji unaopitisha manii unaojulikana kitaalamu kama Epididmorchitis.

Ngiri Kavu (Hernia), aina hii ya ngiri huwapata wanawake na wanaume wote kwa ujumla. Ngiri kavu inapompata Mwanamke huitwa Fermoral Hernia, na pindi inapompata mwanaume inaitwa Scrotal hernia. Kwa maana halisi ya ngiri au mshipa wa ngiri ni hali inayotokea katika mwili wa binadamu ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili. Sehemu hiyo inayoathiriwa mara nyingi huwa ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Pamoja na hivyo mshipa wa ngili hujitokeza sehemu mbalimbali za mwili na hupewa majina tofauti kutokana na sehemu ulipojitokeza, kwa mfano ngiri ya tumbo inajulikana kitaalamu kama Abdominal Hernia, pia watoto wanaozaliwa na vitovu vikubwa inaitwa Umbilical Hernia, na pale ngiri inapojitokeza katika sehemu ya haja kubwa inaitwa Anal Herni. Dalili zake hazitofautiani sana hata hivyo ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote isipokuwa kuna baadhi ya ngili hujitokeza na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa wa mwili wa kupitiliza au kuongezeka uzito kwa ghafla, pia kua na kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.

Mojawapo ya dalili za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
• Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
• Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.

• Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
• Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

======

Ugonjwa wa ngiri ya kitovu (Umbilical Hernia)

Hili ni tatizo la kiafya ambalo huathiri ukuta wa tumbo na kitovu. Tatizo hili husababishwa na mambo makubwa matatu; kwanza ni kasoro ya kuzaliwa. Hapa ni kwamba kitovu kinakuwa na kasoro tangu pale mtoto anapokuwa tumboni kabla hajazaliwa.

Tatizo hili kwa watu wazima lipo mara tatu zaidi kwa wanawake ukilinganisha na wanaume ambapo lipo kwa kiasi kidogo sana. Kwa watoto kiwango cha tatizo hili vinalingana kwa wote wa kike na wa kiume na tafiti zinaonesha kwamba, tatizo ni kubwa kwa watoto wa Kiafrika ukilinganisha na mataifa mengine.

Aina ya pili ya tatizo hili ni ngiri ya kitovu. Hii inatokea tu pasipo na kasoro za kuzaliwa nazo. Hili linatokea kutokana na shinikizo la mgandamizo wa hewa na nguvu ndani ya tumbo kunakosababishwa na unene kupita kiasi, kunyanyua mizigo mizito au vitu vizito mara kwa mara, kikohozi cha muda mrefu na ujauzito wa mimba ya mapacha kwa mwanamke.

Aina ya tatu ya ngiri ya kitovu inaitwa ‘Paraumbilical hernia’. Aina hii ya ngiri hutokea zaidi kwa watu wazima na husababishwa na kasoro upande wa juu wa kitovu kuelekea kwa juu kufuata mstari wa kati wa tumbo.

DALILI ZA UGONJWA
Ngiri hutokea katika eneo la kitovu ambacho kwa lugha nyingine huitwa ‘Umbilicus’, ‘navel’ au ‘Belly button’. Kwa watoto wachanga wanapozaliwa kitovu huwa kirefu sana na huungana na kondo la nyuma la mama ili kupeleka lishe na hewa ya oksijeni kwa mtoto anapokuwa tumboni.

Baada tu ya kuzaliwa, mtoto hujitegemea hivyo kitovu hukatwa katika eneo maalum ili kipungue urefu. Baada tu ya kitovu cha mtoto kupona, mtoto anaweza kupatwa na tatizo hili la ngiri ya kitovu tangu anapokuwa mtoto mchanga ambapo akilia kitovu kinatokeza juu na anaponyamaza kinarudi ndani.

Hali hii wakati mwingine humsababisha mtoto apatwe na maumivu makali huku akilia kila wakati.

Aina hii ya ngiri huwa haipasuliwi kwani huisha yenyewe baada ya miaka miwili hadi mitatu, lakini baada ya umri huo kama haikuisha basi mtoto atafanyiwa upasuaji kurekebisha.

Endapo mtoto ngiri hiyo itakuwa inamsumbua kabla ya umri wa miaka mitatu, basi hatapasuliwa bali itafanyiwa utaratibu wa kuirudisha kitaalam ili isiendelee kutokeza na kuleta maumivu. Ngiri inapokuwa kubwa, tundu lake huwa haliongezeki hivyo husababisha matumbo na kila kitu kitachomoza na kubana nje kushindwa kurudi ndani na kusababisha hali iitwayo ‘Strangulation’.

Kama hali hii haitatibiwa mapema basi italazimika upasuaji wa dharura na ikichelewa huweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa. Tatizo hili hutokea hata kwa ngiri nyingine ambazo tutakuja kuziona katika matoleo mengine.

UCHUNGUZI
Ngiri ya kitovu huonekana kwa macho pale inapochomoza ambapo dhahiri itaonesha imechomoza, wakati mwingine mgonjwa atalalamika maumivu na kama ni mtoto atakuwa analia mara kwa mara.

Vipimo vingine vitategemea na daktari kadiri atakavyoona inafaa.

MATIBABU
Matibabu ya ngiri ni kupasuliwa, haishauriwi kufungia sarafu kwani inaweza kukosewa na kusababisha sehemu ya utumbo kubanwa au kuleta maambukizi ya ngozi kwenye kitovu. Kwa mtoto huisha yenyewe taratibu na ikibidi hupasuliwa baada ya umri wa miaka mitatu.

Wakubwa ni lazima ipasuliwe kama inaleta shida. Wahi hospitali ya mkoa kwa uchunguzi na tiba

======

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).


Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). 

Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

No comments: