Thursday, October 12, 2017

JIFUNZE MADHARA NA TIBA YA TEZI DUME PAMOJA NA SARATANI YA TEZI DUME

Baada ya mgonjwa kujihisi dalili zilizotajwa, daktari atamfanyia uchunguzi wa mwili kabla ya kumfanyia vipimo zaidi.
Image result for UGONJWA WA TEZI DUME NA MATIBABU YAKE
Vipimo vinaweza kutofautiana kati ya mgonjwa na mwingine, lakini baadhi ya vipimo ni pamoja na:
-Kuchunguza tezi dume kupitia njia ya haja kubwa au Digital Rectal Examination (DRE): Hiki ni kipimo cha kwanza ambacho mgonjwa hufanyiwa na daktari wake.
Ni kipimo kinachoweza kumpa daktari picha ya tatizo na kufahamu kuhusu ukubwa na hali ya tezi dume. Daktari akiwa amevaa glovu huingiza kidole chake cha shahada katika njia ya haja kubwa au puru  ya mgonjwa, kisha kuzungusha zungusha ili kufahamu kama tezi limevimba ama la, na pia hali yake kama ni gumu kuliko kawaida ama lina utando na nyama laini.
-Kipimo cha damu cha Prostate-Specific Antigen (PSA): PSA husaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH. PSA ni aina ya protini inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo kuna saratani ya tezi dume.
-Utrasound ya Puru (Rectal Ultrasound): Kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH. Utrasound ya puru pamoja na kuonyesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH.
-Kiwango cha utokaji wa mkojo (Urine Flow Study): Ni kipimo kinachotumika kufahamu kasi ya utokaji wa mkojo. Mkojo unaotoka kwa kasi na kiwango kidogo huashiria kuwepo kwa BPH.
-Kipimo cha kuchunguza kibofu cha mkojo (Cystoscopy): Kipimo hiki husaidia kuweza kufahamu ukubwa wa tezi, sehemu tezi lilipobana njia ya mkojo na kiwango cha kubana huko. Aidha, huwezesha pia kutambua hali ya kibofu cha mkojo ikoje.
Uwezo wa kufanya tendo la ndoa
Wagonjwa wengi waliofanyiwa upasuaji wa BPH huhofia kuhusu uwezo wao wa kufurahia tendo la ndoa baada ya upasuaji. Kwa kawaida, huchukua muda fulani kwa agonjwa kuweza kurejea hali ya kawaida ya kufurahia tendo hilo.
-Hisia: Madaktari wengi husema kuwa iwapo mgonjwa aliweza kupata hisia muda mfupi baada ya upasuaji, uwezo wake wa kuendelea kupata  hisia ni mkubwa zaidi.
Hata hivyo, iwapo mgonjwa hakuwa na uwezo wa maumbile yake kusimama awali, upasuaji wa tezi dume hauna uwezo wa kumrejeshea uwezo wake.
-Kutoa mbegu: Ingawa wanaume waliofanyiwa upasuaji wa tezi dume bado wanaweza kupata mdiso, mara nyingi upasuaji huu huwafanya wawe wagumba ,yaani wasioweza kupata watoto.
Hali hii kwa kitaalamu huitwa Retrograde Ejaculation au kilele (mshindo) kikavu. Kwa kawaida, wakati wa tendo la ndoa, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo.
Wakati wa tendo la ndoa, misuli maalum hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume.
Hata hivyo, upasuaji wa BPH huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Mbegu  hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.
-Kufika kilele : Huwa hakuna tofauti kubwa ya kufika kilele  kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.
BPH na Saratani ya Tezi Dume:
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja, ingawa baadhi ya dalili za BPH zinafanan na zile za saratani ya tezi dume, kuwa na BPH hakuongezi uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume.
Hata hivyo, mwenye BPH anaweza pia na saratani ya tezi dume bila saratani hiyo kugundulika, ama wakati huo huo au siku za baadaye. Hivyo, inashauriwa kuwa, ni vema wanaume wote kuanzia miaka 40 na keundelea kufanya uchunguzi wa tezi dume zao walau mara moja kila mwaka.
Matibabu
Matibabu ya BPH yameganyika katika sehemu mbili, yale yanayofanywa kwa kutumia dawa na yale yanayofanywa kwa kutumia upasuaji mdogo.
Aidha, matibabu hufanywa kwa watu wenye BPH kubwa zaidi na dalili zinazowaletea usumbufu na kuathiri maisha yao, wakati wale wenye dalili ndogo ndogo hawalazimiki sana kuhitaji matibabu.
Matibabu kwa njia ya dawa
Dawa hizi hutumika kwa lengo la kulifanya tezi dume kusinyaa na kupungua ukubwa wake. Dawa hizo ni pamoja na:
-Finasteride na dutasteride ambazo huzuia uzalishaji wa homoni ya DHT. Matumizi ya dawa hizi husaidia kuzuia kukua na kuvimba kwa tezi dume au kulifanya tezi dume kusinyaa kabisa kwa baadhi ya wanaume.
• Terazosin, doxazosin, tamsulosin na alfuzosin husaidia kulainisha misuli ya tezi dume na hivyo kupunguza mbano wa mrija wa urethra, hali inayosaidia mkojo kutoka vizuri.
Matibabu kwa njia ya Upasuaji
Upasuaji mdogo (Minimal Invasive Procedures)
Upasuaji mdogo husaidia kuondoa dalili za BPH na hufanyika pale ambapo matibabu kwa njia ya dawa yameshindwa kuonesha mafanikio yeyote. Njia hizo ni:
-Tiba ya kutumia mawimbi ya joto (Transurethral Microwave Procedures, TUMT): Tiba hii hutumia kifaa kinachotoa mawimbi ya joto (microwave) yanayochoma na kuharibu tishu zilizovimba za tezi dume. Matibabu huchukua chini ya saa moja na yanaweza kufanyika bila mgonjwa kuhitaji kulazwa.
-Tiba ya kutumia sindano maalum (Transurethral Needle Ablation, TUNA): Njia hii hutumia visindano vidogo ambavyo huunganiswa kwenye chombo chenye kutoa nishati ya joto kuunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
-Tiba ya kutumia joto la maji (Water-Induced Thermotherapy): Tiba hii hutumia maji ya moto yaliyochemshwa kwa kifaa maalum  kuunguza na kupunguza tishu zilizovimba za tezi dume.
Upasuaji mkubwa
Madaktari wengi hushauri kuondolewa kabisa kwa tezi dume iwapo itathibitika kuwa mgonjwa ana BPH.
Zipo njia nyingi za upasuaji wa BPH, nazo ni pamoja na upasuaji kwa kupitia kwenye mrija wa mkojo (Transurethral Surgery, TURP), upasuaji mkubwa wa wazi (Open Surgery), upasuaji wa kutumia nishati kuondoa tishu za tezi dume (Laser Surgery), na upasuaji wa kutumia joto la Fibreoptic Probe kuchoma tishu za tezi dume (Interstitial laser coagulation).

No comments: