Thursday, October 5, 2017

KAMANDA MAMBO SASA ANENA HAYA KUTOKANA NA TUKIO LA WATU 10 KUFA BAADA YA KUNYWA GONGO ENEO LA KIMARA

Watanzania wameshauriwa kutumia vinywaji vilivyothibitishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) ili kuepukana na matatizo yanayopatikana katika vinywaji hivyo kwa kuwekwa vitu kama sumu na hata madawa mengine yasiyofaa kwa bidamu katika utengenezaji wa vinywaji hivyo.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam ndugu Lazaro Mambosasa alipokuwa akitoa ripoti ya watu kumi waliofariki baada ya kunywa kinywaji aina ya gongo maeneo ya kimara jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda Mambosasa alisema kuwa upelelezi wa awali unaonyesha kuwa waliofariki ni 10 na siyo 19 kama vyombo vya habari vilivyoripoti jana na eneo la tukio ni Kimara stop over na muuzaji alikuwa ni marehemu mama Anoza na katika eneo la tukio zilikutwa chupa 3 za ujazo wa lita moja moja inayodhaniwa ni pombe ya moshi(gongo).

Aidha kamanda huyo alieleza kuwa watu hao waliofariki ni Maleo Ramadhani mwenye umri wa miaka 45 ambae alifariki baada ya kupelekwa mwananyamra hospitali na alipopata nafuu alirudi nyumbani na ndipo umauti ulipomkuta , na wapili ni mmasai aliyefahamika kwa jina moja la Yona anayekadiliwa kuwa na miaka 20 hadi 30 alikuwa mlinzi wa getini kwa jamaa aliyeitwa Paula Kisanga mkazi wa Kimara stop over.
Na taarifa nyingine zilizopatikana zinaonyesha kuwa kuna watu wengine nane waliofariki dunia kwa kunywa pombe hiyo na miili yao ipo Mwananyamara na  hospitali ya Tumbi Kibaha Mohamedi Issa miaka 67 mkazi wa Kiamra Saranga, Kabugi Rashid miaka 64 mkazi wa Saranga, Stanslaus Joseph miaka 58 Kimara Saranga, Stephen Isaya miaka 61 Kimara Saranga, Monica Rugaillukamu miaka 42 mkazi wa Kimara Saranga, Alex Madega miaka 41 mkazi wa Kimara Korogwe, Hamisi Mbala miaka 35 mkazi wa Kimara Golani, Eksoni Nyoni miaka 28 mkazi wa Kimara stop over,


Lakini pia vielelezo vyote vinapelekwa kwa mkeamia mkuu ikiwa ni chupa na miili ya marehemu hao ili kufanyiwa uchunguzi na kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo, na huku jeshi la polisi likifanya msako mkali kumbaini aliyewauzia pombe watu hao,

No comments: