Thursday, October 26, 2017

LAAC YAIPONGEZA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KUPUNGUZA HOJA ZA CAG

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es  Salaam Isaya Mwita akijibu hoja ya  kamati ya  Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa LAAC mjini Dodoma leo ambapo kamati hiyo imeipongeza jiji la Dar es Salaam kwakupunguza hoja kwa CAG.
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

KAMATI  ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) i imeipongeza  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupunguza hoja za ukaguzi katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Pongezi hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Vedastus Ngombale baada ya kamati hiyo kupitia Ripoti ya hesabu za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Hata hivyo, Ngombale amesema halmashauri hiyo imeshindwa kuthibitisha mchango wake katika mfuko wa wanawake na vijana kwa mwaka wa fedha 2014/15 na mwaka wa fedha 2015/16.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2014/15 halmashauri hiyo ilitakiwa kuchangia Sh 10 milioni na mwaka wa fedha 2015/16 11 sh 11 milioni.
“Halmashauri inaagizwa kuwasilisha udhibitisho wa malipo hayo katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kabla ya Novemba 30 mwaka huu,”amesema.
Kamati hiyo pia iliishauri halmashauri hiyo katika kuepuka kujirudia rudia na upendeleo wa fedha za mfuko na kwamba iweke utaratibu maalum utakokuwa
na ugawaji wa fedha hizo kwa usawa.

LAAC  iliishauri pia halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inaandaa vitabu vinavyopelekwa katika kamati hiyo kwa usahili ikiwa ni pamoja na kuweka uthibitisho wa nyaraka kwa kila hoja inayoibuliwa na (CAG).
Akizungumza mbele ya kamatimhiyo , Mstahikk Meya wa jiji la  Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema  kuwa mwaka jana walipofika katika kamati hiyo walikuwa na hoja nyingi lakini mwaka huu wanafarijika kutokana na kuwa na agizo moja ambalo wataenda kulifanyia kazi haraka.
“Tamanio langu mwenyekiti ni kumaliza hoja na tubaki kuja kupata ushauri tu,   nadhani tunaweza kuwa ni halmashauri ya kwanza kuwa na agizo moja tu,”amesema.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana amesema agizo hilo litatekeleza kabla ya Novemba 30 na ushauri walioupata wataufanyia kazi.

No comments: