Friday, October 6, 2017

MSIGWA AMJIBU IGP SIRRO SAKATA LA DEREVA WA LISSU

Baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumtaka kwa mara nyingine dereva wa Mbunge Tundu Lissu, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amemjibu Mkuu huyo wa Jeshi kwamba kutangaza hadharani kumtaka dereva huyo ni kinyume na
Image result for MSIGWA
Msigwa amefunguka hayo ikiwa ni siku moja baada ya IGP Sirro kutangaza akiwa Mtwara kwamba dereva huyo ndiye ambaye anakwamisha upelelezi wa shambulio la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mh. Msigwa amesema kwamba anaamini dereva wa Lissu anastahili kuhojiwa lakini pia kutokana na hali ya usalama wa maisha yake ilikuwa lazima apelekwe nje ya mipaka kutokana na aina ya tukio na siyo kuitwa polisi siku ya pili kwa kutumia vyombo vya habari kwani ni kumuweka pia hatarini dereva huyo.

"Naendelea kuamini dereva wa Tundu Lissu ambae ni 'first physical witness' lazima atahojiwa.., na lazima atatoa ushirikiano wake kama ambavyo alijitahidi kumsaidia Lissu kabla na baada ya kupigwa risasi.. hivyo lazima atatoa ushirikiano wake, kwa uhitaji huu wa polisi, mnaonesha umma kwamba dereva wa Lissu ni mtuhumiwa mkuu kwenye issue hii" - Msigwa.

Ameongeza kwamba "Dereva wa Tundu Antiphas Mughwai Lissu anaitwa Simon Mohammed Bakari yuko Nairobi kwa sasa, porojo za awali kwamba ametoweka na hataki kuonekana ni ujinga wa kupuuzwa, yuko Nairobi akiendelea na huduma za kisaikolojia, yupo kwenye mikono salama. Alishuhudia tukio na kuokoka kimiujiza.., kutokana na hali ya usalama wa maisha yake ilikuwa lazima apelekwe nje ya mipaka...jamaa walitaka kuondoa uhai wa wote wawili..., Mungu ni mwema sana.., siku zote na hata milele.., they survived to tell the tale" alisema Msigwa 

Mbali na hayo Mbunge Msigwa ameendelea kufunguka kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba "Tundu Lissu akipata nafuu na kurejea kwenye hali  yake nae atahojiwa.., ndivyo ilivyo.., na ulimwenguni kote kuwa uchunguzi wa matukio ya kihalifu  hatua zinafanana. Lissu yupo hai na atasema yote.. atamtaja kama dereva ni mhusika. Acheni kufinyanga hili suala..

Aidha Msigwa amesema kwamba dereva wa Lissu alistahili kupatiwa ulinzi kutokana na tukio la shambulio la bosi wake aliloshuhudia" Msigwa amefafanua.

"Huyu dereva alipaswa kupewa ulinzi na usalama wa maisha yake.., pia kwa sababu ameshuhudia tukio la mtu wake wa karibu.., hakuna sababu za kwanini aitwe siku ya pili baada ya tukio kubwa la uhalifu wa maisha ya binadamu kwa kupitia vyombo vya habari. Sikutaka kuamini kama angelitoa ushirikiano wa kutosha kwa nyakati zile.., labda sasa anaweza. Tusitumie vyombo vya habari kuitana kwenye upelelezi wa polisi na kutaja yupi anatakiwa na yupi ameachiwa., bado tension ni kubwa sana kwenye jamii" Msigwa.

No comments: