Friday, October 13, 2017

Mwita ayapongeza mashirika ya UNICEF, SAWA kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya kisasa mapya ya vyoo.


MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambaye pia ni Diwai wa Kata ya Vijibweni Isaya Mwita amelipongeza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Dunia UNICEF kwakufadhili na kukamilisha ujenzi wa majengo matatu mapya  pamoja na ukarabati wa majengo mawili ya vyoo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Vijibweni leo katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 15, Meya Mwita amesema  {UNICEF] kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la  Sanitation and Water Action [SAWA} wamewezesha ujenzi huo na kwamba itasaidia kupunguza uhaba wa matundu ya vyoo.
Meya Mwita amesema pamoja na shukrani hizo lakini bado kuna vipaumbele vingi ambavyo vinatakiwa kukamilika lakini kutokana na uhaba wa fedha inawia vigumu na hivyo kuwaomba wasiishie hapo bali waendelee kufadhili miradi mingine.
Ameongeza kuwa tatizo la vyoo mashuleni imekuwa ni changamoto kubwa hivyo pamoja na msaada huo, kama Meya wa jiji na Diwani wa kata hiyo ataendelea kushirkiana na wananchi ili kuwezesha na kuhamasisha shule nyingine ziweze kuwa na matundu ya vyoo.
“ Nisema na washukuru sana,mmefanya kazi kubwa, lakini msiishie hapo, leo hii mpo kwenye kata ya Vijibweni, lakini zipo shule nyingi ambazo zinauhaba wa vyoo, nitumie nafasi hii kuwaomba tena,lakini pia na wadau wengine ambao wanaweza kutusaidia katika hili” amesema Meya Mwita.
Aidha katika hatua nyingine amewahakikisha walimu wa shule ya msingi Vijibweni kuwa kutokana na changamoto za hofidi za walimu katika shule hiyo hadi kufikia Agosti 2018 atakabidhi ofisi shuleni hapo.
Aliongeza kuwa kazi ya maendeleo katika jiji la Dar es Salaam linawezeshwa kwa ushirikiano wa wananchi na viongozi wao, hivyo akawaomba kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zile ambazo zinaweza kutatuliwa na wao wenyewe.

“ Kwenye mambo ya  maendeleo, Serikali inaendelea kufanya kwa nafasi yake, lakini pia wazazi tusaidiane katika ujenzi wa shule ,mimi Diwani wenu, Meya wenu wa jiji, kuna eneo la heka saba  tumepata kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, ambapo kuanzia mwaka kesho tutaanza kujenga shule” amesema Meya Mwita.
Kwaupande wake Mtaalamu wa huduma za Maji, Afya na usafi wa Mazingira wa UNICEF ,John Mfungo amempongeza Meya Mwita kwa ushirikiano wake tangu kuanza kwa mradi huo nakusema kuwa alikuwa akitumia muda mwingi na mwananchi wake kuonyesha ushiriki na hivyo  kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huo.
Aidha amesema kuwa ni muhimu kuendeleza jitihada za kuboresha mazingira katika shule kupitia utoaji wa huduma bora za maji, afya na usafi wa mazingira.

Hata hivyo ujenzi wa miundombinu hiyo imefanikishwa kwa ufadhili wa shirika la UNICEF na kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya SAWA,Manispaa ya Temeke, Diwani wa kata ya Vijibweni ,uongozi wa wazazi shule ya msingi Vijibweni.

No comments: