Hospitali na
zahanati za manispaa ya kigamboni zimeendelea kufanya vizuri katika utoaji wa huduma
za afya hadi kufikia kuwa na kiwango cha nyota tatu japo kuwa halmashauri yake
bado ni changa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoDr. Faustine Ndugulile akizindua kituo cha afya cha Pemba Mnazi wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam. |
Hayo yamesemwa
mapema leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia, wazee na
watoto Mh. Faustine Ndugulile alipokuwa akizindua kituo cha afya cha Pemba Mnazi
kilichopo halmashauri ya manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Katika uzinduzi huo wakazi wa eneo hilo walipata
nafasi ya kutoa kero zao mbele ya naibu waziri na miongoni mwa malalamiko hayo
ni upungufu wa Zahanati, vifaa tiba kama mashine za X-ray pamoja na Outro sound,
magari ya wagonjwa, mashimo ya kutupia taka taka n.k
Lakini pia changamoto nyingine ni ubovu wa bara bara hali inayofanya kushindwa kupitika wakati wa mvua pamoja na upungufu wa watumishi katika kituo hicho alichokizindua leo kwani kina jumla wa watumishi wawili ambao ni mganga mmoja na muuguzi mmoja.
Akijibu maswali
ya wakazi hao naibu waziri huyo alisema kuwa kwa sasa tatizo la madawa halipo
kwa zaidi ya asilimia 80 kwani serikali imetenga fedha za kutosha kuhakikisha
dawa zinapatikana katika hospitali za serikali na wagonjwa hawalalamiki tena
kuhusu madawa kwani bohari ya taifa ya madawa ina dawa za kutosha.
Lakini pia
Dr. Faustine alisema kuhusu tatizo la umeme ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa
manispaa kuwasiliana na mkurugenzi wa Taneso ili jumatatu waje wafanye tathini
ya kiwango gani kinahitajika ili atoe na huduma hiyo iendelee kupatikana
kituoni hapo.
Aidha naibu
waziri huyo aliendelea kusema kuwa hospitali ya Vijibweni pale ilipo ni padogo
hivyo kuna eneo lililotengwa kwa ajiri ya ujenzi wa hospitali hiyo na mwakani
mwanzoni ujenzi huo utaanza na kwa vifaa tiba kama X ray ataongea na wizara
yake mpaka mwakani mashine hizo zitakuwepo ili kuepuka tatizo la kwenda mpaka
wilaya nyingine kufuata huduma hizo.
No comments:
Post a Comment