Wakazi wa
maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wanaoishi maeneo ya karibu na mito
pamoja na mabondeni wametakiwa kuacha tabia za kutupa taka taka, kuchimba
mchanga na kuunganisha chemba za vyoo katika maeneo hayo.
Hayo
yamesemwa mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Poul Makonda
alipokuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo yaliyoathiriwa na mvua
kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Mkuu wa mkoa
huyo alisema kuwa wananchi ni vema kuacha tabia hiyo kwani wanapotupa taka au
kuchimba mchanga katika mito kwani hali hii inasababisha maji kukosa muelekeo
hivyo kuingia katika makazi ya watu.
Lakini pia
kwa chemba za choo zinapounganishwa katika mito hiyo inasababisha magonjwa ya
mlipuko kama kipindu pindu na magonjwa mbalimbali ya matumbo.
Aidha Mh.
Makonda alipenda kuwasihi wananchi wa maeneo hayo ya mabondeni kuishi kwa
tahadhari kwani kama unahisi kwako si salama ni vema ungehama mapema kwani
utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuanzia tarehe 1 ya mwezi ujao mvua itakuwa
kubwa zaidi ya hii.
Lakini pia
alisema kuwa kwa wilaya moja ya kinondoni peke yake zimebomoka nyumba zaidi ya
190 na nyingine zaidi ya 200 zimevamiwa na maji, hivyo kuwataka wnanchi wawe
makini na hali hiyo kwani ni hatari kwa maisha yao.
Mkuu wa mkoa
huyo alipokuwa akiongea na wananchi wa kawe alisema kuwa uhalibifu uliofanywa
na maji na kuharibu daraja la Malichela, ameshaongea na jeshi la wananchi na
karibuni unaanza ujenzi wa daraja la muda mfupi kipindi ambacho Tanroads
wanajipanga kwa ajili ya kutengeneza daraja la muda mrefu.
Aliongezea
kwa kusema kuwa zaidi ya billion moja zimetolewa na benki ya dunia kwa ajili ya
mradi wakupasafisha na kurekebisha eneo la jangwani hivyo wapo katika mchakato
wa kuelewana na Injinia na mpaka wiki ijayo kazi hiyo itaanza rasmi.
No comments:
Post a Comment