Leo octoba
11 ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani shirika
lisilo la kiserikali la Health Promotion Tanzania (HDT) linaungana na asasi
mbalimbali za kiraia, wadau wa elimu na jamii kwa ujumla kuiomba serikali
kuwekeza zaidi katika elimu ya mtoto wa kike.
Lakini pia
uwekezaji huu uende sambamba na kulinda haki za mtoto wa kike ikiwa kumlinda na
ndoa pamoja na mimba za utotoni, ukatishaji wa masomo wa aina zote pamoja na
ukatili wowote anaoweza kufanyiwa mtoto wa kike.
Na kutokana
na hili kumesababisha kuundwa kauli mbiu inayosema “ondoa vizuizi vya kujamii,
kitamaduni, na vile vya kimiundo mbinu ili kufanikisha usawa katika elimu ya
sekondari na chuo kwa mtoto wa kike.”
Akiongea na
waandishi wa habari mapema leo meneja wa miradi ya utetezi wa HDT Bw. Greysmo
Mutabashoby alisema kumekuwa na vizuizi vingi katika swala la upatkanaji wa
elimu kwa mtoto wa kike ikiwemo ukosefu wa mabweni katika shule za kata na vyuo
kati, lakini pia changamoto ya usafiri na umbali wa shule na vyuo ivyo kufanya
watoto hawa kukata tama na kukatisha masomo yao.
Meneja huyo
aliendelea kwa kusema kuwa Takwimu zinaonyesha kwa Tanzania kwa wasichana wa
umri wa kati ya miaka 10 na 19 ni asilimia 18 ya watanzania wote, ripoti ya
maendeleo ya serikali kwa mwaka216 inaonyesha udahili wa wasichana katika shule ya msingi ulizidi
wa wavulana kwa asilimia 0.1 lakini wa wavulana kwa sekondari ulizidi wa
wasichana kwa asilimia zaidi ya 6.1 hii inaonyesha tunahitaji nguvu ya ziada
katika kupinga hali hii.
Vyanzo
vingine vinaonyesha kuwa zaidi ya wasicha 550,000 walikatishwa masomo baada ya
kuapata ujauzito nah ii ni kwa muongo mmoja uliopita, lakini pia takwimu za
(TDHS-MIS) kwa mwaka 2010 zinaonyesha asilimia 27 ya wakina mama wote
waliojifungua walikuwa ni wasichana chini ya miaka 20.
Bw. Greysmo
aliendelea kwa kusema kuwa kuna mila na desturi potofu ambazo zinapaswa
kukemewa kwa nguvu zetu zote ambazo ni kama ndoa za utotoni, ukeketaji, ubaguzi
wa kijinsia na kupendelea jinsia ya kiume mfano mfumo dume na nyingine za aina
hii, ambazo zinambana na mtoto wa kike na kumfanya akose haki zake za msingi
kama taarifa kuhusu afya yake na kusababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni.
Na mwisho
shirika hilo lilitoa mapendekezo yafuatayo kwanza kabisa kuiomba serikali
kufanya mapitio na kubadilisha sharia na sera kandamizi kwa mtoto wa kike
ikiwemo sharia ya ndoa ya mwaka 1977 na kuweka umri wa motto wa kike kuolewa ni miaka 18 badala ya 14 inayotumika
hivi sasa.
Lakini pia
serikali kuondoa vizuizi kwa mtoto wa kike na kutengeneza mazingira ya usawa
ambayo yataweza kuhamasisha upatikanaji sawa wa elimu kwa mtoto wa kike na
wakiume.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za watu binafsi pamoja na waandishi wa habari wakisikiliza kwa umakini mawasilisho mbalimbali kutoka kwa viongozi HTP. |
Wazazi nao
kwa nafasi yao kuchukua hatua ya malezi bora yenye tija kwa motto wa kike na
kuondoa dhana ya upendeleo, lakini pia kwa watoto wa kike kuweza kupambana na
changamoto zinazowakabili na kuwasihi wasiingie katika mambo yaliyo tofauti na
umri waona kuwataka wasome kwa manufaa yao ya baadae.
No comments:
Post a Comment