Monday, October 9, 2017

TECNO YAZINDUA DUKA JIPYA (SMART HUB) MLIMANI CITY DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu nchini TECNO imezindua duka kubwa zaidi la simu za mkononi “TECNO SMART HUB” lenye ukubwa wa mita za mraba 110, duka hilo lenye uwezo wa kuhudumia takribani wateja zaidi ya 50 kwa mara moja.


(Menea Daniel Xu akizindua na kuwakaribisha wadau wa TECNO)

Nia ya TECNO SMART HUB hii kubwa ni kutoa huduma zote zinazohusu simu za mikononi za kisasa yaani “smart phones” ikiwemo simu zenyewe na vifaa vyake kama vile chaja, klabu za watumiaji wa TECNO, nahuduma kwa wateja ya papo kwa papo.

Wakati wa uzinduzi huo, meneja wa kampuni ya simu za TECNO Bw. Daniel xu, aliongoza wateja waliofika kushuhudia uzinduzi wa SMART HUB HIYO kukagua na kujionea uzir  wa duka duka  hilo jipya huku akitoa maelezo kwa wageni walioalikwa kazi mbalimbali  za vitengo vilivyomo katika duka hilo, TECNO imezindua duka hili maalumu ili kuwapa wateja wake huduma bora na za kisasa Zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu wa biashara za simu za mkononi nchini.

Aidha wateja pamoja na wageni waalikwa wali furahia kuhudhulia uzinduzi huo baada ya kupata elimu ya jinsi ya kutunza simu za kisasa “smart phones” vizuri hasa kwa watumiaji wapya wa simu hizo. Lakini kwa sasa TECNO wameweza kuweka mafundi wao kwenye TECNO SMART HUB hiyo kubwa, ambapo pia wanatoa huduma za ushauri pamoja na kutengeneza simu kwa ustadi wa juu kabisa  endapo simu ya mteja itakua  na tatizo lolote.

Uzinduzi wa TECNO SMART HUB, uliendana sambasamba na burudani za aina mbalimbali ikiwemo muziki na vinywaji vilivyotolewa bure kwa wateja wa TECNO waliofika katika eneo la tukio. 

Kampuni ya simu za TECNO, ndio kampuni inayo ongoza kwa kutoa simu za kisasa zenye ubora wa hali ya juu pamoja na huduma bora zaidi, kuliko kampuni yoyote nchini. Na kupitia duka lao hilo utafurahia ulimwengu wa simu bora za kisasa uliojaa huduma bora za kujali wateja.

Mwonekano Smart hub:
(Muonekano wa duka jipya la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City)


    (Eneo la mapumziko na vipuli/accessories za simu)

(Wateja wakipata maelezo juu ya bidhaa mpya ya SPARK katika duka la TECNO SMART HUB)



(Mteja akipata maelekezo na ufumbuzi kutoka kwa mtoa huduma wa TECNO)

    (Sehemu ya duka, eneo la display za simu)

  Sehemeu ya wateja kupumzika wakusubiri huduma

No comments: