Friday, October 6, 2017

TGNP MTANDAO YAWAPA TUZO ZA HESHIMA MADEREVA WA TRENI WANAWAKE

Wanawake kote nchini wametakiwa kuwa na ujasiri wa kupingana na mfumo dume kwa kufanya kazi ambazo zinafanywa na wanaume kwani hakuna ugumu katika kazi yoyote endapo utaipenda na utakuwa na nia ya kuifanya kazi hiyo.
Afisa habari wa TGNP Mtandao Bi. Monica John kulia akimkabidhi zawadi ya tuzo ya heshima Bi. Theresia Bernard kwa kuwa mwanamke pekee wa pili kuendesha treni nchini Tanzania
Hayo yamesemwa mapema leo na Theresia Bernad Mahagatira ambae ni dereva wa pili katika historia ya nchi yetu kuendesha treni, walipokuwa wakikabidhiwa tuzo za heshima yeye pamoja na Ritha Chibombo kwa kuwa wanawake pekee kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu.

Wanawake hao wamepokea tuzo hizo mapema leo jijini Dar es salaam walizokabidhiwa na Afisa habari wa TGNP Mtandao Bi. Monica John makao makuu ya shirika la reli la Tazara ikiwa ni katika mpango wa kuendelea kuenzi michango ya wanawake waliofanya mambo makubwa katika nchi yetu.
Bi. Theresia Bernard akionyesha Tuzo yake ya heshima juu baada ya kukabidhiwa na afisa habari wa TGNP Mtandao 
Tuzo hizo zimetolewa kwa Bi. Theresia Bernad kwa kuwa kinara kwa kuendesha treni kwa zaidi ya miaka 14 toka mwaka 1982 mapaka 1996 akiwa ni dereva, na Bi. Ritha Chibombo Mduma yeye akiwa ameendesha treni kwa zaidi ya miaka 9 toka 2006 mpaka sasa akiwa bado dereva wa treni hilo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hizo Bi. Theresia alisema kuwa wao walipanza walikuwa wanne kulikuwa na wakwanza ambaye yeye alishindwa na wapili ni yeye na yupo mpaka sasa hivyo anahesabiwa kuwa ni wakwanza baada ya wa kwanza kushindwa na wengine wawili waliobaki kufariki dunia.
Afisa habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Monica John kulia akimkabidhi tuzo ya heshima Bi. Ritha Chibombo Mduma kwa kuwa ni miongoni mwa madereva wachache wanawake wa treni 
Aidha Bi. Theresia aliendelea kwa kusema kuwa kwa sasa yeye ni regional controller na siyo dereva hivyo uendesha mara moja moja sana majukumu yake ni kuhakikisha kuwa treni zinakwenda ama kufika kwa wakati, kuwa na mawasiliano mazuri na vituo vingine ili kuhakikisha usalama wa chombo na abiria.

Alipenda kusisitiza kwa kusema kuwa changamoto kila sehemu zipo ila sio za kuwafanya wasichana kuiongoapa fani hiyo ya kuendesha treni na miongoni mwa changamoto hizo ni kukosa usingizi kwani muda mwingi unautumia kufanya kazi lakini pia kupata ajari pamoja na kuwa mbali na familia yako kwa kipindi kirefu hivyo watoto kukosa malezi ya mama.
Tuzo zilizotolewa mapema leo ofisi za Tazara jijini Dar es salaam
Na mwisho alipenda kuwashauri wanawake kujishughulisha na shughuli zote na kuachana na dhana ya kwamba hizi ni kazi za wanaume kwani kama yeye sasa amekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa kuwa watu wengi wanamshangaa kwa kumuona akiendesha chombo hicho na wengine utamani kuwa kama yeye na kuwasihi wanawake kuwa na uthubutu.


No comments: