Leo ikiwa ni tarehe 13 mwezi octoba ni Siku
ya kufunga mradi wa miaka mitano uliolenga kupunguza athali za saratani
ya mlango wa kizazi kwa wanawake wa kitanzania.
Mradi huu uliojikita kwenye uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na utoaji wa matibabu ya awali, ulitekelezwa kwa kiasi kikubwa na Marie Stopes Tanzania, PSI/Tanzania na UMATI.
Katika
kipindi cha miaka mitano cha utekelezaji wa mradi, vilianzishwa vituo 79 katika
mikoa 22 nchini Tanzania na watoa huduma za afya 210 wakapatiwa mafunzo ya
utoaji wa huduma hiyo.
Kwa
uwezeshaji uliofanywa na Taasi ya Bill and Melinda Gates, mradi uliweza
kuwafikia takribani wanawake 187,267 waliopata huduma ya uchunguzi na wanawake
7,602 wakipatiwa matibabu.
Kaimu
Mkurugenzi wa kitengo cha afya ya uzazi kilichopo chini ya wizara ya afya
amesema; “Saratani ya mlango wa kizazi ni tatizo kubwa Tanzania. Kwa ushahidi
uliopo, saratani ya mlango wa kizazi inaongoza kwa kusababisha madhala na vifo
vitokanavyo na saratani kwa zaidi ya miaka kumi. Katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road ambacho ni kituo pekee cha saratani Tanzania, inaonesha kuwa
asilimia 38 ya wagonjwa wapya wa saratani waliopokwa katika kitengo hicho mwaka
2015 walikuwa ni wa saratani ya mlango ya kizazi. Takwimu hizi zimetokana na
takwimu za usajili wa wagonjwa Katika
taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Amesema,
“wizara imeweka juhudi kubwa katika kupambana na saratani ya mlango wa kizazi
nchini, mipango inayoendelea inalenga pia kuimarisha miradi ya saratani ya
matiti na saratani ya tezi dume. Pia wamepiga hatua katika kuhakikisha wanaboresha
upatikanaji wa huduma ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na matibabu
yake nchini. Kwa sasa kuna vituo 466 vinavyotoa huduma ya uchunguzi wa saratani
ya mlango wa kizazi na matibabu ambavyo ni hospitali zote za mkoa na wilaya
nchini, na baadhi ya vituo vya afya na zahanati.
Ameongeza,
“Licha ya jitihada hizi zinazoendelea bado hatujaweza kukidhi mahitaji hata
kufikia asilimia 10, wanawake wachache sana wamepata huduma ya uchunguzi hasa
kwa wanawake walio maeneo yasiyofikika kirahisi. Kwa sababu hii, wizara ya afya
maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto inaahidi kuwezesha juhudi za
kuboresha na kukuza huduma za saratani ya mlango wa kizazi ikijikita zaidi katika
huduma za msingi za kinga na uchunguzi wa mabadiliko ya awali ya saratani hii.
Wizara
ikiwezeshwa na GFF imenunua mashine 100 za kutoa tiba ya mgando ya mabadiliko
ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi (cryotherapy) na mashine 9 za matibabu
ya juu ya mabadiliko hayo ya awali (LEEP) ili kuboresha upatikanaji wa huduma
ya uchunguzi na matibabu katika vituo 90 nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Marie Stopes Tanzania amesema, “mradi huu umetuacha na mafundisho
mengi ambayo yanaweza kutumiwa na wadau
mbalimbali wanaotekeleza miradi ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi
nchini Tanzania na amewataka wadau kutumia elimu hii iliyotokana na uzoefu wa
kazi iliyofanywa na MST, PSI na UMATI badala ya kusumbuka kubuni vitu ambavyo
tayari vimefanywa na mashirika haya.
Alifafanua
kuwa majaribio ya utaratibu wa kutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya kizazi
kwa kwa utaratibu wa huduma ya mkoba kwa kutumia kipimo cha HPV / DNA umekuwa
ni wa ufanisi na kuwa ni utaratibu wa kwanza kufanikiwa duniani wa kuhakikisha
mama anafanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu siku hiyo hiyo kwa kutumia
care-HPV™ katika nchi zinazoendelea.
Baadhi ya washiriki kutoka Hospitali, Taasisi mbalimbali pamoja na waandishi wa habari walioudhuria semina hiyo. |
No comments:
Post a Comment