Wednesday, October 18, 2017

WANAWAKE WAFANYA BIASHARA WA MIPAKANI KUPEWA ELIMU YA JINSIA NA TGNP MTANDAO

Leo tarehe 18 ya mwezi octoba ni ufunguzi wa semina ya siku tatu iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa lengo la kuwakutanisha wafanya biashara wanawake wa mipakani pamoja na maafisa mbalimbali wanaofanya kazi kwenye mipaka ili kuweza kuzijadili changamoto zinazowakabili wanawake hao na namna ya kuzitatua.
Katika semina hiyo iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 35 wakiwemo wafanya biashara wanawake wa mipakani na wadau wa asasi mbalimbali za kiraia na maafisa wa serikali kama TRA, TBS, SIDO, TWCC na wengine wengi.

Akiongoza semina hiyo kwa wanawake wafanyabiashara wa mipakani Beatrice Hazekiel alisema lengo ni kujengeana uwezo na uelewa wa dhana muhimu za jinsia na kuhakikisha mipakani wanapofanyia shuguli zao kuwe na uwiano sawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake katika maamuzi na mambo mbalimbali yanayohusu jinsia.
Lakini pia muwezeshaji alisema ili kuweza kuwa na usawa wa kijinsia ni lazima watu kuondoakana na dhima potofu ya mfumo dume ambao unatumika kuwanyanyasa wanawake na wananchi walio wanyonge katika taifa letu na kuonekana kuwa baadhi ya watu kuwa ni wanathamani kushinda wengine hivyo kuwanyonya wanyenge hao.

Muwezeshaji huyo aliendelea kwa kusema kuwa mfumo dume unajengeka au kulindwa na makuzi yetu na wanawake wengi huona kama ni wakosaji na hawakuwa wanastaili kuwepo walipo kwa kuona ni makosa yao wenyew lakini sio makosa yao ila ni makuzi toka walipoanza kukua na kujengewa mfumo wa kuwa wewe ni mtoto wa kike majukumu yako ni kupika kuosha vyombo na kulea ila mtoto wa kiume yeye anatakiwa kusoma ilia je kuwa na maisha mazuri hapo mbeleni.
Lakini pia hata kwa upande wa kiuchumi pia ipo hivyo kwani mwanamke anatakiwa kukaa nyumbani lakini baba ndio anatakiwa kutafuta pesa na hata mama akitafuta basi inakuwa ni ya familia nzima siyo ya mama peke yake kama ilivyo kwa baba, na hivyo hivyo hata katika masomo ilikuwa hivyo hapo nyuma kwa kuambiwa wewe mtoto wa kike unatakiwa usome masomo rahisi kama ya arts na ukionekana unasoma masomo ya sayansi unaambiwa unasoma masomo ya kiume.

Aliendelea kwa kusema kuwa jambo lingine ni fikra mgando na hii ni kwa wale ambao wamejiwekea kwamba huyu mwanamke basi kuna vitu hawezi kuvifanya kama kufanya biashara au mwanamke kugombea uongozi anaonekana kama astahili wakati ni vitu ambavyo anaweza kuvifanya, lakini pia kwa wanawake wenyewe kukubali kuwa kuna baadhi ya kazi ni za wanaume hivyo wao hawawezi kama ukandalasi, urubani na vitu vingine vingi hivyo ndio vinaitwa fikra mgando.
Aidha muwezeshaji huyo alisisitiza swala la uwezeshaji wanawake na kusema kuwa ni vema kuwawezesha wanawake na wasichana kuzitambua fursa chache walizo nazo katika jamii yao na kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha hali hiyo, na kuwapa nguvu ya kushiriki katika maamuzi na hata kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.


Na mwisho kabisa aliongelea bajeti yeye mlengo wa kijisia na kusema kuwa hii ni bajeti shirikishi nan i yenye kulenga makundi yote katika ngazi zote za jamii bila kumuacha hata mmoja nyuma ikiwa walemavu, wazee na watoto vijana wakina mama na makundi yote yaweze kufikiwa na bajeti hii ili kuondoa tatizo la kuonekena imeelemea upande mmoja.

No comments: