Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii akiwa nyumbani kwake na amepelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis imesema Zitto amekamatwa asubuhi hii Masaki wilayani Kinondoni, akidaiwa kutoa kauli za uchochezi wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi wilayani Temeke juzi.
Pia kukamatwa huko kwa Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini ,kuna kuja ikiwa ni wiki moja kupita baada ya Rais John Magufuli kuvitaka vyombo vya usalama kuwamata watu wanaotoa takwimu tofauti na serikali yake na kuwachukulia hatua kupitia sheria ya Takwimu ya mwaka 2014 ambayo inatoa hukumu kwenda jela hadi miaka miwili kwa mtu anatoa Takwimu tofauti.
Agizo hilo la Magufuli ambalo alikumtaja jina mtu, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kauli hiyo ilikuwa inamlenga Zitto ambaye mara kwa mara amekuwa mkosoaji mkuu wa serikali ya Magufuli kwa kusema hali ya uchumi wa nchi ni mbaya huku akitoa takwimu mbali mbali ambazo zinaonesha hali hiyo ya uchumi.
No comments:
Post a Comment