Monday, November 20, 2017

JE WAJUA KUNA HATARI KIASI GANI KWA MJAMZITO AKILALIA MGONGO?

Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Tokeo la picha la mjamzito kulalia tumbo
Utafiti wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito.
Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto.
Watafiti wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawafai kuwa na tashwishi yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao.
Takriban mimba 225 nchini Uingereza huishia mtoto kuharibika na watafiti wa utafiti huo wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo wanawake wataendea kulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto.
Utafiti huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida la Kujifungua ni mkubwa wa aina yake na unathibitisha tafiti ndogo nchini New Zealnd na Australia.

No comments: