Tuesday, November 21, 2017

JENGO LA CLOUDS MEDIA LAUNGUA MOTO ANGALIA PICHA ZA MOTO HUO...

Kampuni ya Clouds Media Group ambao ni wamiliki wa Clouds Fm, Clouds Tv pamoja na Choice Fm yenye makao makuu yake Mikocheni jijijni Dar es salaam.
kampuni hiyo imepata ajari ya moto uliyoanza sehemu ndogo ya studio na ulikuwa ukienea sehemu mbali mbali lakini kwa sasa juhudi zinaendelea kuzima moto huo alisema Ruge ambae ni Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group.

Aliongeza kwamba kituo hicho si mara ya kwanza kupatwa majanga ya moto ambapo mara ya kwanza walipokuwa katika jengo la Kitegauchumi eneo la Posta jijini Dar es Salaam, moto uliteketeza studio zao na kupoteza vitu mbalimbali ambapo moto wa leo umeteketeza baadhi ya ofisi za studio ya Televisheni.
Hata hivyo, alikishukuru kikosi cha Zimamoto kwa kufika haraka eneo la tukio na kuuzima moto huo.  Vilevile alisema hakuna binadamu aliyepata madhara kutokana na tukio hilo.
Mutahaba alisema juhudi zaidi zinaendelea katika kituo hicho ili kurekebisha mambo yaliyotokea na kwamba ratiba zao zitaendelea kama kawaida.

No comments: