Wednesday, November 8, 2017

JUMUIYA YA VIJANA WA BAKWATA WAMPONGEZA MUFT ABUUBAKARI ZUBERY KWA UTENDAJI KAZI WAKE NDANI YA MIAKA MIWILI TANGU KUPATA CHEO HICHO

Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu BAKWATA Taifa,  inampongeza Muft wa Tanzania Sheikh Abuubakar Zubery bin Ally kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika uislamu kwa miaka miwili aliyohudumu katika cheo hicho tangu tarehe 10 Septemba 2015.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika eneo la Masjid Al Ghadir Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Sheikh Othman Zuberi amesema tangu alipochaguliwa Muft Abubakar mwaka 2015 ameweza kufanya mambo mbalimbali baada ya kutoa maelekezo kwa viongozi wa dini ikiwemo kudumisha amani, kuunganisha jamii,  kuleta maendeleo, ushirikiano mzuri wa Baraza na Mashirika ya Dini ya ndani na nje ya nchi, kuamrisha mema na kukataza maovu, uboreshaji wa elimu ya dini na secula, kusisitiza kujitambua, mahusiano mazuri kati ya Baraza na viongozi wa nchi, kukataza kufanya kazi kwa mazoea, na sensa kwa maendeleo ya waislamu ambapo ameagiza kupatikana kwa takwimu sahihi kwa waislamu kupitia misikiti mbalimbali hapa nchini.
Katibu huyo amewatoa hofu waislamu kuhusu suala la sensa kwa waislamu na kuwaambia wasiwe na hofu kwani hata katika kitabu kitukufu cha Qur-an kimewataka waislamu kufanya mambo kwa mahesabu hivyo wamuunge mkono Muft Abubakar kwa kufanya hivyo.

Na kuwapongeza makatibu wa mikoa na Wilaya mbalimbali walioanza zoezi la sensa kwani sensa ni kwaajili ya maendeleo ya waislamu.

Katibu huyo amewataka viongozi  na Taasisi mbalimbali za dini kumuunga mkono Muft Abubakar kwa maendeleo ya waislamu.




No comments: