Wednesday, November 29, 2017

JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA GEITA YACHAGUA MWENYEKITI MPYA

Wajumumbe wa Jumuiya ya wazazi wakiwa kwenye mstaari kwaajili ya kupiga kura wa kumchagua mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa mkoa wa Geita na wajumbe.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Geita ambaye amemaliza muda wake,Doto Biteko akiwashukuru wajumbe kwa ushirikiano ambao walimpatia wakati wa uongozi wake.

Baadhi ya wagombea kwenye nafasi mbali mbali ndani ya jumuiya hiyo.

Wasimamizi wa uchaguzi  wakitambulishwa kabla ya zoezi kuanza.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akijitambulisha mbele ya wajumbe wa mkutano huo.


Mwenyekiti aliyechaguliwa kwenye jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita,Bw Lucas Singu Mazinzi  akiwashukuru wajumbe ambao wamemchagua.

Msimamizi wa uchaguzi   ambaye  ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Donald Magesa  akielekeza namna ambavyo wanatakiwa wajumbe kupiga kura.

Daud Katwale Ntinonu akijitambulisha na kuelezea namna ambavyo ameamua kurudi ndani ya chama ca mapinduzi akitokea chama cha CHADEMA.

Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoani Geita,Joseph Mwita akielezea namna ambavyo zoezi la uchaguzi lilivyofanyika(Picha na Joel Maduka)
Na,Consolata Evarist,Geita


Jumuiya ya umoja wa wazazi wa chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Geita  imefanya  uchaguzi wa mwenyekiti na wajumbe wa mkutano Mkuu ambapo katika uchaguzi huo,Bw Lucas Singu Mazinzi aliibuka mshindi kwa kupigiwa kura 250.


Akitangaza matokeo katika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo    ,msimamizi wa uchaguzi   ambaye  ni Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu Donald Magesa  , alisema kura ambazo zilipigwa ni 320  na ambazo ziliharibika ni 19  kura harari 301.

 Alisema kuwa   ,Lucas Singu   ameshinda dhidi ya wagombea wenzake   Hewa Samweli Masatu  aliyepata kura 36 na Mayengo Simion Kitindi ambaye alipata kura 15.

Aidha Magesa aliendelea  kutaja  nafasi za   wajumbe watakaowakilisha mkutano mkuu Taifa kutoka kwenye jumuiya hiyo, kuwa ni Ibrahimu Jumu Ibrahimu   Kura 38 , John Kafimbi Saulo kura 11, Charles Kazungu Mabeyo kura 192 na Rose Venasi Mweko  55.


Awali mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye amemaliza nafasi yake ya uenyekiti wa jumuiya hiyo Doto Biteko,alisema   ndani ya kipindi chake cha uongozi amejidhatiti katika kuleta maendeleo ndani ya jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na miradi ambayo ni endelevu mfano uwanja ambao upo kwenye Wilaya ya Bukombe ambacho kinatarajia kujengwa chuo na kusimamia shughuli zote za maeneo ya uchimbaji madini ya dhahabu yanayomilikiwa na jumuiya hiyo.

Aliongeza kuwa anaamini ambaye amechaguliwa kurithi kiti chake hataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha pale ambapo ameishia.

Aidha Mwenyekiti wa  jumuiya hiyo ambaye amechaguliwa,Bw  Singu mbali na kuwashukuru wajumbe ambao wamempatia ushindi huo ,alisema mikakati aliyonayo ni kutafuta miradi mikubwa zaidi ndani ya jumuiya ikiwa ni pamoja na kukisaidia chama hicho kutimiza malengo yao.

Pia amewashukuru Wagombea wenzake ambao alikuwa akichuwana nao kwenye kinyanganyiro hicho kwa kukubaliana na matokeo ambayo yametangazwa.

No comments: