Leo ikiwa ni
tarehe 9 mwezi wa 11 Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) likiwa chini ya udhamini wa Shirika
la Maendeleo la Uswidi(Sweden International Development Cooperative Agency–SIDA)
limeandaa kongamano la wasichana lililofanyika mapema leo katika ukumbi wa
Lamada hotel Ilala boma jijini Dar es salaam.
Baadhi ya mabinti wakifanya igizo katika Kongamano la Watoto wa Kike lililoandaliwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF mapema leo jijini Dar es salaam |
Mgeni Rasmi
katika kongamano hilo alikuwa ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo
la Uswidi(Sida) Ms. Carin Jamtin akiwa ameambatana na Mkuu wa Idara ya
Mahusiano na Maendeleo Ms. Ulf Kallsting, lakini pia kongamano hilo liliudhuliwa
na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Maafisa Maendeleo na Ustawi wa
jamii, Walimu, Polisi, Wanafunzi pamoja na wasichana walio nje ya shule.
Akiongea na
waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa CDF Bw. Koshuma Mtengeti alisema
kuwa Kongamano hilo limekutanisha washiriki mbalimbali wakike na wakiume, waathirika
wa mimba za utotoni na hata wale ambao bado wapo mashuleni ili kuwajengea uwezo
wa kulinda na kutetea haki za mtoto wa kike.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) akitoa ufafanuzi wa jambo fulani katika Kongamano la watoto wa kike lililoandaliwa na shirika hilo mapema leo jijini Dar es salaam. |
Na pia lengo
kuu la kongamano hilo likiwa ni watoto wa kike kupata nafasi ya kukutana na Mkurugenzi
Mwanandamizi wa Shirika la Uswidi na kumuelezea mafunzo pamoja na miradi
mbalimbali inayoendeshwa na CDF katika ukombozi dhidi ya mtoto wa kike katika mambo
kama. Ukeketaji, Mimba za utotoni, Ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia pamoja
na kuonesha shughuli za ujasilimali ikiwa ni kama mafanikio ya mradi wa CDF.
Lakini pia
katika kongamano hilo mabalozi wa CDF wanaume na wavulana wamepewa fursa ya
kuelezea namna wanavyofanya kazi zao kama mabalozi na jinsi wanavyojitahidi kuelimisha
jamii juu ya mdahara ya ukeketaji, ukatili wa kijinsia na ndoa pamoja na mimba
za utotoni.
Mkurugenzi huyo
aliendelea kwa kusema kuwa Polisi, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa jamii na
viongozi wengine wa serikali wamepata nafasi ya kuonyesha ni kwa namna gani
wameweza kufanya kazi na kushirikana na CDF katika kulinda na kutetea maslahi na
haki za mtoto wa kike.
Akiongea
katika kongamano hilo Mkurugenzi Mwandamizi wa shirika la la maendeleo la Uswidi(SIDA)
Carin Jamtin, amesema shirika lao limekuwa likitetea haki za watoto kwa
kuhakikisha watoto wakike na wakiume wanakuwa na haki sawa katika jamii
hususani haki ya kupata elimu.
No comments:
Post a Comment