Sunday, November 19, 2017

MASAUNI AZINDUA ZOEZI LA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA MARA

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wakati wa hafla  iliyofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, mkoani Mara.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Masawe (katikati), wakishuhudia uchukuliwaji wa alama za vidole za mmoja wa wananchi waliofika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, mkoani Mara kuandikishwa kwa ajili ya kupata kitambulisho cha utaifa. Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiingiza taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa, baada ya kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho hivyo leo Mkoani Mara.Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiakisi fomu ya taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa, baada ya kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho hivyo leo Mkoani Mara.Kupitia zoezi hilo wananchi wa mkoa huo na wilaya zake watapata fursa ya kupata vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Masawe (kulia),wakiteta jambo baada ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), kuzindua zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo,mkoani Mara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa tayari kuhudumia wananchi waliofika katika zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa baada ya kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo,mkoani Mara. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments: