Friday, November 10, 2017

Meya Mwita asema mkutano wa COP 23, utatoa suluhisho la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi.


NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI.

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa  mkutano wa COP 23 ambao Mameya na watendaji wakuu wa majiji na miji mbalimbali duniani utatoa  suluhisho la pamoja la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi katika miji yao.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi , Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana wa kwanza kulia wakijadiliana jambo na ujumbe wa jiji la Hamburg katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia ya Nchini unaoendelea Nchini Ujerumani.
Akiwa Nchini Ujerumani , Meya Mwita emesema kuwa mkutano huo  utakuwa mahususi kwa jiji la Dar es asalaam kupata suluhisho na kuhakikisha kuwa wanakabiliana  ipasavyo na mabadiliko  ya tabia ya nchi ikiwemo janga la mafuriko ambalo limekuwa ni tatizo sugu jijini hapa.

Mkutano huo unaofanyika sambamba na Mkutano wa 23  wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, COP 23  inahusu miji na Taasisi zenye uhusiano na ubia na miji ya Ujerumani katika utekekezaji wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko hayo inayofadhiliwa na Nchi hiyo.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita katikati mwenye koti jeusi  ,akiwa na Mkurugenzi wa jiji Sipora  Liana wakipata chai baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mkuanomhuo.
Mkutano huo  wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi umeandaliwa na Taasisi ya Engagement Global ya Ujerumani kwa miji washirika kutoka nchi mbalimbali duniani ambapo  umeanza jana alasiri mjini Bonn nchini  Ujerumani.

Kutoka Tanzania miji mingine inayoshiriki katika mkutano huo ni Jiji la  Mwanza, Manispaa ya Zanzibar na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.   
Hata hivyo mkutano huo utaendelea hadi Novemba 11, mwaka huu ambapo    jiji la Dar es Salaam linashiriki katika likiwa na ujumbe wake unao ongozwa na Mstahiki Meya Jiji hilo  Mwita pamoja na  Mkurugenzi  Sipora Liana. 

No comments: