Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo kwa
Mkuu wa Wilaya ya Geita(Wakwanza kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Nguzombili wakati wa ziara yake katika Shule hiyo.
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiingia ndani ya moja ya darasa lililojenjwa chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya Msingi Nguzo Mbili. |
Vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita. |
Mkuu wa Mkoa
wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Geita kwa
kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyo chini ya mpango
wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo mbili.
Akizungumza
wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert Gabriel alisema kuwa
ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi wa madarasa kwa
ubora wa hali ya juu katika shule hiyo.
" Inashangaza sana kuona maeneo mengine
wanatumia fedha zote kiasi cha shilingi 20 milioni katika ujenzi wa darasa moja
lakini kuna mapungufu mengi hivyo lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha
katika miradi ya Serikali"Alisema Lughumbi.
Akiwa
shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia vikundi vya
ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa pia
kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa serikali na hatimaye fedha
zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika huduma za jamii.
Katika hatua
nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka uongozi wa Shule ya Msingi Nguzo
Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa miundombinu hiyo ambayo mingine
imeanza kupasuka.
Aidha, ameagiza shule
hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo vilivyojengwa vianze kutumika
badala ya kufungwa.Pamoja na kutembelea Shule ya Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa
Mkoa pia ameitembelea shule ya Sekondari na kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya
madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo.
Shule ya
Msingi Nguzo mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia shilingi milioni 13 kwa
kila darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya kisasa pamoja na ukarabati wa
madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na fedha iliyobaki katika bajeti ya
darasa moja.
Mkoa wa
Geita una upungufu wa vyumba vya madarasa 8600 hivyo serikali imeandaa mpango
kabambe wa kutokomeza tatizo hili kwa kushirikiana na jamii na wadau wote wa
Mkoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Imeandaliwa na mtandao wa maduka online.
No comments:
Post a Comment