Katika kuunga
mkono juhudi wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Pombe Magufuli ya kuwa
na uchumi mkubwa wa viwanda, taasisi isiyo ya kiserikali ya Mamas and Papas for
Community Reform inawakaribisha wakazi wa jiji la Dar es salaam na maeneo ya
karibu katika maonyesho ya bidhaa yatakayofanyika eneo la Kigamboni jijini Dar
es salaam.
Maonyesho
hayo yatakayodumu kwa siku tatu mfurulizo kuanzia tarehe 30 mwezi huu wa 11
mpaka tarehe 2 ya mwezi 12, taasisi inapenda kuwakaribisha Wafanya biashara,
Wafugaji, Wajasiliamali, na wenye viwanda vikubwa na vidogo kuja kushiriki
katika maonyesho hayo pamoja na kuleta bidhaa zao.
Lakini pia maonyesho
hayo yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiserikali, wakidini, na taasisi
binafsi ili kuweza kubadilishana uzoefu katika kukuza viwanda vyetu, na pia
maonyesho hayo yanatarajiwa kuanza saa 2 kamili asubuhi katika viwanja vya Machava
vilivyopo wilaya mpya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Hivyo kwa
wote wanaopenda kujitangaza kupitia maonyesho haya basi wanatakiwa kufika
viwanja vya Machava na kujisajiri kwani usajiri ni bure kabisa na usajiri
utafanyika kuanzia tarehe 15 mpaka tarehe 25 ya mwezi wa 11.
Na pia
ikumbukwe kuwa maonyesho hayo yanaongozwa na kauli mbiu inayosema “Fursa mikononi
mwako 2017 Wilaya ya Kigamboni kwa pamoja tunaweza”
Mamas and Papas
for Community Reform ni taasisi inayojishughulisha na utoaji wa elimu ya
kupinga matumizi ya dawa za kulevya, ndoa na mimba za utotoni, watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi, Ukimwi, Malaria na elimu ya Ujasiliamali na ina Makao
Makuu yake Kigamboni jijini Dar es salaam.
Imetolewa afisa habari wa Mamas and Papas for Community Reform Moshi Said
No comments:
Post a Comment