Kampuni kinara ya simu za mkononi TECNO imeungana na Vodacom kutambulisha toleo jipya
TECNO Phantom 8, Simu hiyo iliyozinduliwa nchini Dubai imetambulishwa rasmi
nchini Tanzania katika duka la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City mapema
mwezi huu.
Akizungumza wakati wa utambulisho
, Afisa mahusiano wa TECNO , Eric
Mkomoya amesema ‘’ TECNO tumeitambulisha
rasmi Phantom 8 nchini Tanzania leo tukiwa na mshirika wetu wa matoleo ya
Phantom nchini , Vodacom .Tumetengeneza
simu bora yenye hadhi, tunayofuraha kuwataarifu wateja wetu kuwa Phantom 8
inapatikana katika Smart Hubs za TECNO na maduka yote ya Vodacom nchini.’’
Alihitimisha
(Image: Mkuu kitengo cha mahusiano
Vodacom Jackline)
Phantom 8 ina
6GB RAM,Betri yake ina uimara wa
3500 mAh za kuhifadhi chaji kwa muda
mrefu, 64 GB ROM, inayoipa simu uwezo wa
ziada wa kuhifadhi data kufikia
2TB , Inavuta picha iliyombali kwa ukaribu bila kupoteza muonekano halisi mara 10 zaidi ya simu za kawaida .
Phantom 8 ina muundo na mtindo wa kuvutia hasa rangi yake yenye mng’ao wa
almasi
(Image: Afisa mahusiano Eric Mkomoya
na Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline)
Ushirikiano baina ya TECNO na
Vodacom umekua wa kudumu ambapo awali waliitambulisha Phantom 6 na 6+ sasa
wanakuletea Phantom 8 inayotikisa soko ikiwa na 20MP kamera ya mbele na 12MP +13 MP
kamera zake 2 za nyuma.
Mwandishi wa habari Asia Matona
alijinyakulia zawadi ya Phantom 8 kwa hisani ya TECNO na Vodacom.
(Image: Mwandishi wa habari Asia
Matona akifurahia zawazi yake ya simu TECNO Phantom 8 aliyoshinda. )
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na
TECNO tafadhali tembelea tovuti yetu ya http//www.tecno-mobile.com
No comments:
Post a Comment