Katika kuhakikisha kuwa
wanaisaidia Jamii inayowazunguka shirika lisilo la kiserikali la The Foundation
Foundation for civil Society limejipanga kuwasaidia watoto wenye matatizo ya
vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatikana katika Taasisi ya mifupa MOI jijini
Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa shirika hilo kuadhimisha siku yao maarufu
ya “GIVING TUESDAY” ambayo hutumia siku hiyo kuisaidia jamii.
Akieleza mikakati ya
kuadhimisha siku hiyo kwa mwaka huu mwakilishi kutoka shirika hilo Ndugu Karin
Rupia amesema kuwa baada ya kuona changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto
wanaohudumiwa katika taasisi hiyo wameamua kuitumia siku hiyo kuwasaidia watoto
hao huku akiwataka watanzania kuwaunga mkono katika kutekeleza Jukumu hilo.
Mwakilishi huyo amesema
kuwa shughuli hiyo itafanyika kwa siku mbili ambapo siku ya kwanza itakuwa
tarehe 25 Novemba ambapo wataitumia kuchangia damu kwa ajili ya watoto hao wenye
matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ,zoezi ambalo litafanyika ndani ya
taasisi hiyo ya Mifupa MOI kuanzia saa tatu asubuhi hadi majira ya mchana
Katika zoezi la pili
litafanyika tarehe 28 Novemba ambayo ndiyo siku maalum ya Jumanne ya kutoa
“Giving Tuesday” ambapo katika siku hiyo shirika limejipanga kusaidia watoto
katika kuwapatia mahitaji mbalimbali ambapo shughuli kubwa itakuwa ni
kuwasaidia watoto kupata upasuaji ambapo amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa
wanasaidia watoto mia moja kupata huduma hiyo ya upasuaji.pamoja na kuwadaia
vifaa mbalimbali vitakavyosaidia katika kwa watoto hao ambapo watanzania wametakiwa
kujitolea kuchangia kwa kasi ili kusaidia shirika hilo kufikia malengo hayo.
Ili kushiriki katika
zoezi hilo la kuchangia damu kwa ajili ya ,kuwa unaweza kupiga simu namba
0762767237.
Video ikifafanua kuhusu
siku hiyo ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday”
No comments:
Post a Comment