Monday, December 11, 2017

Meya Mwita ahudhuria mkutano wa Viongozi wa serikali za mitaa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa huko Addis Ababa

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameondoka Jijini hapa jana jioni kuelekea  Addis Ababa, kuhudhuria mkutano wa kujadili changamoto zinazo wakabili viongozi wa serikali za mitaa.
Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo unalengo la kujadili na kutoa majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo Mameya wote.

Miongoni mwa changamoto ambazo zitajadiliwa katika mkutamo huo pamoja na mambo mengine ni  suala la bajeti katika halmashauri na ukusaji wa mapato.

Mbali na Mameya ,mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka Nchi mbalimbali.
Aidha Meya Mwita atazungumza na mkutano huo kuelezea changamoto zilizopo katika jiji la Dar es Salaam , namna ambavyo  kwa asilimia kadhaa wameweza kuzitatua.

Aidha katika mkutano huo ataeleza pia mafanikio yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam kupitia sekta mbalimbali za Maendeleo.

" Katika mkutano huo hatuta kuwa jiji la Dar es Salaam pekee ,ni Nchi mbalimbali Duniani zitakuwepo, tutajadili changamoto zinazo tukabili kwenye halmshauri zetu, mafanikio,lakini pia kujengeana uwezo kwenye utendaji kazi" alisema Meya Mwita.

                         

No comments: