Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekunua taarifa ya kukamata watu wanaovaa vimini na kunyoa mtindo wa kiduku.
Hatua hiyo inakuja baada ya gazeti la kila siku la Nipashe January 17 (leo) kutoka na kichwa cha habari; Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa viduku.
Akizungumza Dar es Salaam Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani mwandishi ameandika kitu ambacho hakukisema.
“Nilitaka nitoe ufafanuzi nikikanusha haya ambayo yameandikwa hayakusemwa na Jeshi la Polisi, anayasema mwenyewe mwandishi kwa interest yake na sana alichokuwa anatafuta ni umaarufu wa stori,” amesema.
“Ninamtaka sasa arudi kwa watanzania aombe radhi ili kuondosha usumbufu uliojitokeza, nimepigiwa simu kuanzia jana toka maeneo mbali mbali kwa jambo ambalo kimsingi halijafanywa na Jeshi la Polisi,” amesisitiza.
No comments:
Post a Comment