BARAZA la Vijana wa Chadema (Bavicha), limesema wimbi la kuhama kwa viongozi na wanachama wa chama hicho, unakipa nafasi ya kujirekebisha na kujipanga vizuri ikiwamo kubaki na wanaofuata misingi ya chama.
Katibu Mkuu Bavicha, Julius Mwita
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa, Julius Mwita akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua kauli ya Bavicha kuhusu wimbi la kung'atuka kwa viongozi na wanachama wa Chadema na kujiunga na CCM).
Amesema “Ni fursa kwa Chadema kuachana na wale wasiofuata misingi ya chama hicho na kubaki na wale wanaofuata misingi ili kutimiza dhamira na lengo la uwepo wa Chadema,” amesema Mwita.
Ameongeza “Lakini leo wanatoka watu ndani ya Chadema wanaenda CCM kwa kauli moja tu wanaunga mkono juhudi za Rais Mgaufuli, sasa siyo jambo geni na siyo jambo jipya kwetu Chadema, tunaona ni fursa ya kukirekebisha chama.”
Anasema wanaojiunga na CCM hawana fikra za kusaidia taifa ni kwa ajili ya tumbo na ndiyo maana wanazunguza vitu vinavyohusiana na fursa
Amesema kuna siasa za namna tatu ambazo ni tumbo, moyo na akili ambapo ameeleza kuwa kama ukifanya siasa zote utakuwa Chadema na ukifanya ya tumbo utakwenda CCM.
Na Abraham Ntambara,
No comments:
Post a Comment