Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (wkawanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Shanes Nungu, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na
Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Morogoro leo Januari 17, 2018. Bw. Kalonga alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Eric Shitindi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Eric Shitindi, akifungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake. |
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora
kwa wadau, hususan katika kipindi hiki ambacho Mfuko unategemea ongezeko kubwa
la waajiri na wafanyakazi, kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa
kujenga uchumi wa viwanda, ambao utaongeza ajira.
Hayo
yamesemwa leo Januari 17, 2018 mjini Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku
tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na
Uamuzi (CMA), ili kuongeza ujuzi kwenye utekelezaji wa majukumu ya Tume.
“Katika
jambo hili la kujenga uchumi wa viwanda, makampuni mengi yataanzishwa, kutakuwa na
waajiri wengi, ongezeko la wafanyakazi, kwa hivyo unategemea kwamba hitajio la
utoaji huduma za Mfuko kwa wadau litaongezeka
na Mfuko umekuja wakati muafaka na tupo kwa ajili ya kuwahudumia wale wote
watakaopatwa na majanga mahala pa kazi lakini pia kuelimisha.” Alisema Bw. Mshomba.
Bw.
Mshomba alisema, kuanzia Julai, 2016 Mfuko
ulianza kupokea madai ya Fidia yanayotokana na kuumia au kuugua mahali pa kazi.
“Jambo
hili si rahisi kwa sababu ndio linaanza kwa hivyo tunahitaji ushirikiano wa
karibu sana kutoka kwa wadau mbalimbali mkiwemo ninyi CMA, na katika hilo
ushirikiano tu hautoshi Mfuko umekuwa ukitoa elimu ili kuwawezesha watu wajue Mfuko umeanzishwa kwa sababu gani, kazi
zake, lakini pia kujua taratibu za kudai fidia pale mfanyakazi anapopatwa na
majanga ya kuumia au kuugua wakati akitekeleza wajibu wake wa kikazi.” Aliongeza
Bw. Mshomba.
“Ndio
maana leo hii tunao wataalamu wetu watakaotoa mada mbalimbali zikiwemo, Sheria
za Fidia, Namna Fidia inavyolipwa lakini shughuli za Mfuko.” Alibainisha
Mkurugenzi Mkuu Bw. Mshomba.
Aidha
aliishukuru Tume kwa kuwashirikisha WCF ili kuwaelimisha wafanyakazi wake kutoka
mikoa yote ya Tanzania bara.
“Ni
muhimu kwetu sisi kuwaelimisha wadau kuhusu shughulim zetu na ndio maana huwa
tuko tayari wadau wetu wanapotualika ili kutoa elimu hiyo.” Alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa ……..kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Bw. Eric F. Shitindi amewahimiza
washiriki wa kuzingatia elimu watakayoipata kwenye mafunzo hayo ili hatimaye
watekeleze ipasavyo malengo ya serikali ya awamu ya nne ya kujenga uchumi wa kati
ifikapo mwak 2025.
“Ni
matarajio yetu kwamba Tume na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, mnao wajibu
mkubwa sana katika kufanikisha azma hiyo ya serikali kama nyinyi mtatekeleza
wajibu wenu.” Alisema.
Baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki.
Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Edrisa Mavura, akitoa hotuba yake.
Maafisa wa CMA wakiteta jambo.
Bw. Mshomba, (kulia), na Bw.Nungu, wakijadili jambo.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, akikaribishwa na Wakurugenzi wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia) na wa CMA, Bw.Shanes Nungu, alipofika kufungua mafunzo hayo
Bw. Mshomba akijibu baadhi ya maswali ya washiriki kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya washirtiki wakifuatilia mafunzo.
Kamishna wa Tume, Bi.Suzanne Ndomba, (kulia), akizungumza kwenye mafunzo hayo. Wengine ni Makamishna wenzake, kutoka kushoto, Bw.Kibwana Njaa, Bw.Jones Majura na Bw.Jaffary Ally Omar.
Picha ya pamoja.
Bw. Mashomba akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalam Omar.
Washiriki wakipitia vipeperushi vya WCF.
No comments:
Post a Comment