Wednesday, February 21, 2018

CDF YAENDELEA KUWANOA WASICHANA TARIME KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA


Kambimbi Kamugisha kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime akitoa Mafunzo kwa Watoto wa kike ambao wamekumbwa na changamoto mbalimbali likiwemo Swala la Ukeketaji, Mimba za Utotoni, Ugumu wa Maisha
 na Changamoto za Familia, 

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa MCN uliopo Tarime yamejumuisha wasichana kutoka kata tano Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Mji, kata hizo ni Nkende,Matongo, Mwema, Manga na Susuni.

Kambibi amesema kuwa wamewapatia Mafunzo ya Ujasiriamali Mabinti hao ili waweze kuanzisha biashara zao kwa lengo la kuendesha maisha huku Shirika hilo likiwasaidia baadhi ya vitendea kazi kwa ajili ya kuanzia pamoja na kuwa
mabalozi wa kupinga suala la Ukatili wa kijinsia katika Wilaya ya 
Tarime kupitia kata zao.


Elimu ikitolewa kwa siku Nne katika Ukumbi wa MCN Mjini Tarime Mkoani Mara.
Wasichana mbalimbali kutoka kata tano za Tarime mkoani Mara wakiendelea kusikiliza mafunzo yanayotolewa na muwezeshaji wa CDF.

 Wasichana 60 wamenufaika na Mafunzo hayo ili wawe mabalozi wa kutoa Elimu ya kupiga Vita Ukatili wa Kijinsia.
Kazi ya pamoja baada ya somo.
Somo linaendelea.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwasilisha kazi.




 
 

No comments: