Friday, February 23, 2018

ZITTO AACHIWA KWA DHAMANA YA MANENO YENYE THAMANI YA MILION 50.

Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mh. Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh. 50 milioni na kudhaminiwa na wakili wake, Lazarus Mvula baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Morogoro tangu jana Alhamisi kwa kufanya mkusanyiko bila kibali.
Tokeo la picha la ZITO AACHIWA KWA DHAMANA
Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini.

“Ndugu Zitto ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh50milioni. Anatakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018,” inaeleza taarifa ya wakili wake.

Aidha, Zitto amefungukia mauaji ya Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

No comments: