BIASHARA

INFINIX KUZINDUA SIMU YENYE KAMERA BORAHOT S3 ni toleo jipya kabisa kutoka kampuni ya simu za mkononi Infinix ambalo inatarajiwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha za mbele kwa kutumia kamera yenye mega-pixel 20 yenye teknolojia mpya ya “low-light selfie” inayomuwezesha mtumiaji kupiga picha hata katika mwanga hafifu. Simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwanzoni mwa mwezi April 2018 nchini Tanzania.
 
Pamoja na uwezo mkubwa wa kamera, simu hiyo pia inatarajiwa kuwa na teknolojia za kisasa kabisa za kiusalama kama “FACE ID” na “FINGERPRINT SCANNER” ambazo zinamuhakikishia mtumiaji usalama wa taarifa katika simu yake, vitu ambavyo vinaifanya simu hiyo kuwa moja ya simu bora kabisa kwa sasa.

Vilevile simu hiyo mpya itakuwa na kioo chenye ukubwa wa nchi 5.7 na uwiano 18:9 itakayoifanya kuwa na muonekano wa kisasa zaidi kama na uwezo mkubwa wakutizama video bila kizuizi.
 

Kivutio kingine Katika simu hiyo ni aina mpya ya processor “QUALCOMM SNAPDRAGON” na Android “Orea” vinavyomuwezesha mtumiaji kutumia “application” nyingi kwa wakati mmoja huku ikiwa na betri yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chaji zaidi ya (4000 mAh).

Uzinduzi wa simu hiyo unatarajiwa kwenda sambamba na uzinduzi wa duka kubwa la Infinix jijini Dar es Salaam ambalo litauza bidhaa zote na Infinix pamoja na kutoa ushauri juu ya matumizi bora ya simu hizo.

About habari24 blog

0 comments:

Powered by Blogger.