|
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (kushoto), akiwa ameambatana na
mwenyeji wake mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes (kulia), baada ya
kuwasili ofisi za Yatch Club kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji
majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
|
|
Kamishna wa Operesheni wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (wa pili kushoto), akiwa na
wakufunzi kutoka nchini Ujerumani na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Wakati
wa uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji
majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es
Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
|
|
Mkufunzi kutoka nchini
Ujerumani Bw. Dan Jungingfer (kulia), akitoa maelekezo ya mbinu za uzamiaji
majini kwenye kina kirefu kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Gift
Longwe na Konstebo Baltazari Swai. Wakati wa
uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa
Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto
Na Uokoaji)
|
Mafunzo haya yanayoendeshwa
hapa nchini na Wakufunzi kutoka Ujerumani yana lengo la kuwaongezea Maafisa na
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji weledi katika kukabiliana na majanga ya
mafuriko na kuzama kwa watu majini haswa kwenye kina kirefu.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
No comments:
Post a Comment