Thursday, March 1, 2018

Meya Dar - Mwita mtembelea mwanasiasa mkongwe wa Chadema aliyelazwa Hospital ya Taifa Muhimbili

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita jana alimtembelea nyumbani kwakwe na kisha kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mwasisi na mkongwe wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Victa Kimesela ambaye anaumwa kwa muda mrefu sasa.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam , Isaya Mwita akiwa pamoja na familia ya Kimesela ,wakitoa msaada wa kumpakiza kwenye gari ya kubebea wagonjwa ya hospital ya Taifa Muhimbili jana alipomtembelea nyumbani kwakwe.Kimesela anaumwa na kwa sasa amelazwa katika hospital ya Taifa Muhimbili.
Kimesela ambaye ni miongoni mwa waasisi walioshiriki kuandaa katiba ya chama hicho mwaka 1992, anaugua kwa muda ambapo familia yake ilimueleza Meya Mwita kuwa alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hivyo kuruhusiwa Jumatano iliyopita.

Hata hivyo muda fupi baada ya  Meya Mwita kufika nyumbani  kwa mwasisi huyo, afya yake ilibadilika na hivyo kwa kushirikiana na familia hiyo  walitoa taarifa Muhimbili ili kupatiwa gari ya kubebea wa gonjwa.

Aidha  gari hiyo ilifika na  hivyo Meya Mwita na familia hiyo waliambatana pamoja kumuwahisha kwa mara nyingine hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu awali.

 Kimesema amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Chama hicho, ikiwepo kuwa katibu mtendaji wa chama hicho wakati wa utawala wa Edwin Mtei, katibu mkuu wa muda wakati wa utawala wa Bob Makani na hivyo kumuachia nafasi hiyo Dk.Wilblod Slaa ambaye kwa sasa amestaafu siasa tangu  mwaka 2015.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na mke wa Kimesela , Suzani Kimesela alipomtembekea nyumbani kwakwe jana .



No comments: