Monday, March 19, 2018

UKWELI KUHUSU TETESI ZA KUFUNGIWA KWA KIWANDA CHA DANGOTE CEMENT CHA MTWARA

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanania (TPDC) linawataka Wananchi kupuuza taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba, kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara kimefungwa kutokana na Sababu mbalimbali ikiwemo, kushindwa kwa makubaliano ya mauzo ya gesi asilia baina ya kiwanda cha Dangote na TPDC. 
Tokeo la picha la ALIPO DANGOTE
TPDC inawataarifu wananchi kwamba, imetimiza makubaliano yote ikiwemo mauzo ya gesi asilia pamoja na ujenzi wa mitambo ya kusafirishia gesi asilia hadi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya kiwanda cha Dangote, tangu 2017. 

Aidha taarifa inayosambazwa katika mitando ya kijamii ya mwaka 2016 imepitwa na wakati

Hivi sasa kiwanda cha saruji cha Dangote kinaendela na zoezi la usimikaji wa mitambo yake ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi ujao(Aprili 2018)

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania

No comments: