Monday, March 19, 2018

WAZAZI WALEENI WATOTO WENU KATIKA MAADILI NA TAMADUNI ZA KITANZANIA

 Naibu Katibu Mkuu Wazazi ccm Tanzania bara
Godfrey Mheluka akiwa anawahutumia wananchi waliouthuria katika
kongamano la kujadili maadili mema   na uzalendo  ni ustawi wa Arusha
yetu na Taifa letu  kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya
Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo
lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja
na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi
iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
kamanda wa vijana  UVCCM mkoa wa Arusha  Philemon
Molel maarufu kama Monabani akiongea na wananchi waliouthuria katika
kongamano la kujadili maadili mema   na uzalendo  ni ustawi wa Arusha
yetu na Taifa letu  kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya
Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo
lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja
na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wa sekta binafsi
iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
Habari picha na  Woinde Shizza,Arusha
Wazazi wametakiwa kutimiza wajibu  wao wa kuwalea watoto  kwakufuata
maadili ya Mtanzania na kuacha kuiga tamaduni  za kigeni  ,kwani
baadhi ya tamaduni za kigeni wanazo ziiga zinachangia kusababisha
mporomoko wa maadili katika jamii zetu .
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wazazi ccm Tanzania bara
Godfrey Mheluka wakati akifunga kongomano  la kujadili  maadili mema
na uzalendo  ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu  kwa ujumla
,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM)mkoa wa Arusha ,kongamano ambalo lilishirikisha wananchi
,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa
serikali pamoja na wa sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa
Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha

Alisema kuwa  wazazi wengi wa wamekuwa wanalea watoto kwa kufuata
tamaduni za wenzetu wan chi za nje wakidai kuwa ndio malezi bora kwa
watoto na yakisasa kitu ambacho sio kizuri kwani baadhi ya tamaduni za
wenzetu ukiangalia za kutoka nchi za kimagharibi  zinaporomosho
maadili kwa watoto wetu.
“ukithamini tamaduni za kimagharibi na ukaacha za kwetu na ukamuacha
mtoto nae akathamini tamaduni hizohizo ujue umempoteza mtoto na
umemuaribu kabisa unakuta mzazi anaona mtoto anavaa mlegezo au kimini
badala ya kumkataza anamuacha anaona kuwa wake ndio mjanja huo sio
ujanja ni ujinga ni kumuaribu mtoto unatakiwa umwambie mtoto hivi sio
vyema ivi nikiwauliza wazazi ivi nyie mngelelewa hivyo  au mngelelewa
vibaya je leo mngekuwepo apo mlipo  ni wajibu wetu kuwalea watoto wetu
kwa kufuata utamaduni wetu mzuri wenye maadili ili kuweza kuandaa
viongozi wazuri wa baada na wazazi wazuri wa baadae “alisema Mhekuka

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya  wazazi ccm mkoa wa Arusha
Dr,John Palanjo alisema ni wazazi anatakiwa kutimiza waji wake kwa
mtoto wake huku pia mtoto akitakiwa kutimiza wajibu wake kwa mzazi
,aliongeza kuwa pia niwajibu wa kila mzazi kumfatilia mtotowake na
kujua maendeleo yake mwenyewe na sio kumuachia mwalimu amfatilie au
dada wa kazi amfatilie huku akibainisha kuwa mzazi yeyote asitafute
mchawi wa mtoto wake kwani ,asilimia kubwa ya wazazi wao wenyewe ndio
wachawi wawatoto wao.
Aidha aliwaasa wazazi kutenga mda wa kukaa na watoto wao na kuongea na
kuwaelezea kipi kibaya na kipi kizuri ili kuwawezesha watoto wetu
kukuwa  kwa kuendana  na yale   yanayopendeza kwa jamii inayowazunguka
.

“mimi na imaini iwapo mzazi akijua wajibu wake atakubali hata kidogo
mtoto wake aharibike ,hivyo ni vizuri mzazi utambue  wajibu  wako
umrudie mungu  usali maana ukiwa na hofu ya mungu lazima utamlea mtoto
kwa kufuata kanuni za kimungu”alisema katibu wa  wawazazi wilaya ya
Arusha Christoper Pallangyo

Kwa upande wake mwenyekiti wa wazazi wilaya  ya Arusha Ally Meku
aliwataka baadhi ya wazazi   kupunguza migogoro  ndani ya familia ili
watoto nao wasiige tabia mbaya kwani  wanapoaanza migogo katika
familia wanashindwa kuwale watoto wao na badala yake watoto hao
wanaanza kutangatanga hovyo na kuanza kuiga tabia mbaya.
 baadhi ya viongozi wakiwa wanaimba na kucheza

 baadhi ya viongozi wakiwa meza kuu wanafatilia kongamano
 RTO  wa mkoa wa Arusha Josephy Bukombe nae alikuwepo katika kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wazazi na vijana waliouthuria katika kongamano hilo kufuata maadili ,huku akiwasihi wazazi  kuwakumbusha vijana wao kuvaa kofia ngumu wakati wanapoendesha pikipiki zao pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kutokea mara kwa mara
 mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano hilo
 wanafunzi wa shule ya sekondari ya Edmond Rice nao waliuthuria katika kongamano hilo


  mwenyekiti wa jumuiya ya  wazazi ccm mkoa wa Arusha
Dr,John Palanjo akiongea na wananchi waliouthuria katika kongamano hilo

No comments: