Katika kipindi
cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2017/2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA
imekusanya kiasi cha shilingi Trilion 11.78 ikilinganishwa na shilingi Trilion
10.86 ambazo zilikusanya kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam. |
Akiongea na
waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa kodi wa TRA Bw. Richard
Kayombo alisema kuwa ongezeko hilo ni sawa na ukuaji wa pato kwa asilimia 8.46
Aidha Mkurugenzi
huyo alisema kuwa katika kipindi cha mwezi machi peke yake TRA imekusanya jumla
ya shilingi Trilion I.54, ikilinganishwa na makusanyo ya mwezi machi 2017
ambapo ilikusanya jumla ya shilingi Trilion 1.34 ambapo ni ukuaji wa asilimia
14.49.
Kayombo aliendelea
kusema kuwa mafanikio yote haya yanatokana na juhudi za walipa kodi, viongozi wa
ngazi zote na kampeni kadhaa, pamoja walipa kodi wapya nchi nzima kuwakumbusha
kulipa kodi kwa wakati na kusikiliza malalamiko yao pamoja na kuwajengea
utaratibu mzuri wa kulipa madeni yao ya nyuma.
Mkutano ukiendelea. |
"Katika kipindi hiki tunaendelea na usajili wa walipa kodi wapya wakiwemo wamachinga ambapo kwa wiki hii tupo mkoani Geita, na tunawakaribisha wafanyabiashara wote wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kupewa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) na maafisa wa TRA watasikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi" alisema Kayombo
Na mwisho Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kuhakikisha huduma zinazotolewa ni bora, TRA inaendelea kutoa elimu kwa kila anayestahili alipe kodi kwa hiari na kwa wakati na mwenye malalamiko yoyote juu ya makadirio amuone meneja wa eneo husika akiwa na vielelezo vyake vyote.
No comments:
Post a Comment