Kwa mara ya kwanza msimu wa Tigo
Fiesta 2018 waja na promosheni murwa inayompa mteja bonasi la uhakika
lenye thamani ya hadi mara mbili ya
kifurushi cha intaneti papo kwa hapo.
Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania leo imetangaza promosheni
murwa kwa wateja wote watakaonunua vifurushi vya intaneti kupitia menu
iliyoboreshwa ya *147*00#. Mteja
atapokea bonasi la uhakika papo kwa hapo lenye thamani hadi mara mbili ya
kifurushi cha intaneti atakachonunua katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018.
Akitangaza promosheni hiyo
jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema,
“Kuendana na msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, promosheni hii ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa wateja
wote wa Tigo wanafurahia maisha ya kipekee ya kidigitali huku wakisambaza
matukio ya Tigo Fiesta 2018 mubashara kutoka sehemu yoyote ile ya nchi kupitia
mtandao wenye kasi ya juu zaidi wa 4G+.”
Hali kadhalika, Tigo
inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018
zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Katika mikoa yote ya Tigo
Fiesta 2018, wateja wanapaswa kupiga *150*01#
na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha
kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi
kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja wa Tigo pia watapata faida
zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta
2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi
za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH
500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla.
Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI
kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua
Trivia.
Tigo ni mtandao unaojulikana
kwa promosheni kabambe na ubunifu wa kipekee unaoendana na mahitaji halisi ya
soko, hivyo kuifanya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa wateja wake zaidi.
Kwa hiyo tumejizatiti kuwapa
wateja wetu promosheni bora zaidi katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2018. Tunawakaribisha
wateja wetu kufurahia ofa hizi murwa.
No comments:
Post a Comment