Thursday, April 19, 2018

ASASI ZINAZOFADHILIWA NA UBALOZI WA UFARANSA ZIMEKUTANA DAR ES SALAAM KUFANYA TATHMINI YA MIRADI YAO.



Asasi za kiraia 12 zilizo chini ya ufadhili wa ubalozi wa Ufaransa na kusimamiwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society zimekutana kutathmini miradi kadhaa ya maendeleo ya jamii wanayoitekeleza katika mikoa mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari mach 21, 2019 katika Hotel ya Protea Cortyard iliyopo Oyster bay jijini Dar es salaam, Meneja Uwezeshaji wa FCS Bi. Edna Chilimo amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini na kuona mradi huo umefanikiwa kiasi gani na umekuwa na changamoto zipi, pamoja na kutafuta ufumbuzi ili awamu ijayo waweze kufanya vizuri zaidi.

Aliongeza kuwa mradi huo ulipewa fedha na Ubalozi wa Ufaransa hapa nchini na ulikuwa na programu mbili ambazo PISSCA na DEFI na programu hizo zote zimelenga kujenga uwezo wa mitandao ya Asasi za Kirai na kuboresha baadhi ya maeneo katika jamii. 

Aidha alisema kuwa mradi huo ulikuwa ni wa miaka miwili na huu ni mwaka wa mwisho, Lakini pia ulihusisha asasi 12 za Tanzania bara na uliweza kuleta mafanikio makubwa kwa jamii hasa kwa upende wa afya ya uzazi kwa watoto wa kike na wakiume ambapo watekelezaji wakubwa katika hili walikuwa ni Msichana Initiative.

Aliongeza kuwa kuisha kwa mradi huu siyo mwisho na kuwashauri wadau watengeneze miradi yenye matokeo mazuri yaani inasaidia jamii hasa ile ya watu wa chini na kuongeza ubunifu juu ya kile wanachokifanya ili kuwashawishi wafadhili kwani wafadhili wengi wanapenda kuona fedha wanazotoa zinaleta mabadiliko chanya kwa jamii.

Kwa upande wake Lightness Njau  kutoka Taasisi ya Msichana Initiative alisema kuwa wao waliufanya mradi huo katika wilaya mbili za Mji wa Dodoma ikiwemo Wilaya ya Kongwa na Chamwino, Na walilenga shule mbalimbali za msingi na sekondari katika wilaya hizo, walichokifanya ni  kufungua Clabs mashuleni na katika club hizo 10 zilikuwa za shule za msingi na 32 za shule za sekondari.

Aliongeza kuwa mafanikio waliyoyapata kutoka katika club hizo mpaka sasa ni wasichana katika shule hizo wameweza hata kuzidai na kuzizungumzia haki zao za msingi, Lakini pia wasichana wengi kwenye hizo club wameweza pia kuwaelimisha wenzao ambao hawapo katika club kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

Alisisitiza kuwa kwa hizo wilaya zote mbili pamoja na kata sita waliweza kufungua Kamati za Ulinzi wa wanamke na Mtoto na zimeanza kuleta matokeo mazuri kwa kuwa mpaka sasa taarifa mbalimbali wanazipokea kutoka kwa wanajamii, Lakini pia wanapewa usharikiano mzuri na serikali katika wilaya hizo zote.

Na kwa upande wa shirika la TAWLA wao waliweza kutekeleza mradi huu kwa kufanya kazi katika eneo la ukatili wa kijinsia kwa kuwajengea uwezo Polisi na Wasaidizi wa kisheria pamoja kuwapa msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo vya ukatili.

Lakini pia kufatia mchakato huo zaidi ya wanawake 472 wameweza kupatiwa msaada na wasaidizi wa kisheria katika wilaya ya Bayo na Mpwapwa, Na kwa upande wa polisi walijengewa uwezo kuzitilia uzito kesi za ukatili wa kijinsia na kuhakikisha zinafikishwa Mahakamani pale ushahidi unapokamilika na kuacha tabia ya kuzipuuzia.

Akionge kwa niaba ya Taasisi hiyo Bw. Barnabas Kaniki alisema kuwa changamoto kubwa katika mradi huo ilikuwa muda ni mdogo kwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia haviwezi kumalizika kwa mwaka mmoja au miwili, Lakini pia changamoto nyingine ni fedha zilizotengwa hazikuweza kufanikisha kufika katika kata zote za wilaya hizo.

Na taasisi zilizokuwa zikitekeleza mradi huo ni IWAPOA, Dignity Kwanza, ATFGM, NGONEDO, NGSEN, GLT, TEG, UWZ, TAWLA, TAMWA, Msichana Initiative na CDF.

Meneja Uwezeshaji wa FCS Bi. Edna Chilimo Akiongea na waandishi wa habari juu ya dhumuni la mkutano.


Lightness Njau  kutoka Taasisi ya Msichana Initiative akitoa wasilisho juu ya mradi wao uliolenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule mbalimbali Mkoani Dodoma

Washiriki wakiendelea na mkutano.

Muwakilishi wa Taasisi ya TAWLA Bw. Barnabas Kaniki akitoa mchanganuo juu ya mradi waliyoufanya wao ambapo waliangazia katika kuwakomboa wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano.

Mkutano ukiendelea.

No comments: